Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Lakini katika kuepukana na upweke katika maisha ni kuwa karibu na watu unaowapenda, usifunge mlango wa upendo. Kwa kuongeza ufahamu huu, utapata mwanga katika kutambua maumivu yako ya upweke na kujifunza jinsi ya kukabiliana na woga na maumivu ya kukataliwa.
 
Magonjwa yanaoweza kuambatana na tatizo la unene uliopitiliza


1.Kisukari Shinikizo la damu (hypertension) 2.Kiharusi (Stroke)
3.Magonjwa ya moyo
4.Tatizo la kutopumua vizuri wakati mtu yupo usingizini (Sleep apnea)
5.Vijiwe katika mfuko wa nyongo (Gallstones) 6.Kiwango cha juu cha lijamu kwenye damu (cholesterol ikiwemo triglycerides)
7.Ugonjwa wa mifupa kama yabisi (osteoarthritis). 8.Saratani ya matiti
9.Saratani ya tezi dume (prostate cancer)
10. Saratani ya utumbo mpana pamoja na maeneo ya haja kubwa (Colorectal cancer)
11.Matatizo ya mzunguko na mishipa ya damu kama vile kuvimba kwa vena za miguuni (varicose veins)
 
Kama mtu mwingine amekukosea, ungehitaji akuombe msamaha, Na ungeamua kumsamehe au kutomsamehe. Lakini unapokuwa umefanya makosa , Hatua hizo kwako hazipo wazi. Huenda huamini kuwa unahitaji kusamehewa, Au unafahamu lakini hujui jinsi gani ya kujisamehe, na unajisikia vibaya.
 
Kitu cha kwanza ambacho nakutaka ukifanye ni wewe kufahamu jinsi ya kujikubali jinsi unavyojisikia sasa hivi.

Fahamu kwamba sio kila mtu mwenye kuwa makini au kuwa na uhakika wa kukubali kwamba amekosea, Mara nyingi kila mtu hujiona kuwa yuko sahihi. Kubali kwamba wewe ni aina ya mtu huyo ambaye anaweza kulitambua kosa na kusema kuwa umehusika katika hilo. umefanya kitu kibaya, lakini ndani ya msingi wako , wewe ni mtu mzuri.
 
Tiba ya kuongezeka unene kupita kiasi
Tiba ya tatizo hili ni mhusika kujitambua ya kwamba ana tatizo na kuwa tayari kupunguza uzito. Mabadiliko ya tabia ya mhusika ni muhimu sana, mabidiliko haya yawe ndio mfumo wa maisha yake ya kila siku.

Kupungua uzito na kujilinda au kutunza uzito ulionao baada ya kupunguza uzito ni jambo la msingi sana na inahusisha mazoezi, chakula na madiliko ya tabia ya mtu.
 
Kanuni za kujisamehe mwenyewe ni zile zile ambazo unawasamehe wengine. Unapomsamehe mtu au kujisamehe ni kuachilia . lakini sina maana ya kujifanya unasamehe kumbe ndani umeweka kinyongo Hapana. Msamaha sio udhuru au msamaha wa jujuu. na haina maana kwamba hutaweza kukumbuka. Kusamehe ni kukubaliana na yaliotokea na kupata njia ya kusonga mbele.
 
Kwenye ndoa na familia, wengi huwa wanafanya makosa ambayo ni ngumu kusamehe. Yasiosameheka. Lakini kuna kitu kimoja ukumbuke kuwa wale waliofanya makosa yasioweza kusameheka na wale ambao wamefanya makosa rahisi kusameheka, wote wamefanya makosa.Wote ni wanadamu. Wanadamu wanafanya makosa. Yote ni makosa. Sisi ni viumbe ambao hatujakamilika, na wote tunahitaji kusamehewa.
 
Wote tunajitahidi kutumia mbinu mbalimbali ili kuepuka makosa. Wakati mwingine mbinu hizi hazitusaidii kitu, Wazazi wetu ndio kioo chetu, hawakuweza kufanya vizuri baadhi yao, mitazamo yetu na kujihukumu kwetu au imani zetu .Nakutaka ukae kimya kwa muda na ujisemeshe hivi; ”Nimefanya nilichofanya kwa sababu mimi ni mwanadamu na mwanadamu sio mkamilifu ”
 
Kubali kilichotokea. Elewa jinsi gani na kwa nini kilitokea , Ona picha hio katika hali ya kuachilia. kusamehe, kiwe ni kizuri au kibaya.

Kujisamehe ni kuhitaji utulivu na kuwa na mtazamo mkubwa kwa kila kilichotokea. Umefanya na lazima ushughulikie matatizo yaliojitokeza na ukubali kuwa hutaweza kubadilisha hilo limefanyika na limepita.
 
Fikiria kuhusu kile kilichokufanya ufikie kutenda hivyo, ulikuwa unataka kukutana na kitu gani? Somo gani ambalo umejifunza hapo na huenda ulishaambiwa na wazazi wako. Kuna uzoefu wowote ulionao au imani yoyote? Utakapojua Kwa nini umefanya ulichokifanya utakuwa tayari upo kwenye njia nzuri ya kujisamehe na utakutana na kile ambacho ulikihitaji .
 
Mazoezi -

Mazoezi husaidia kupunguza uzito hasa kipindi cha miezi sita ya mwanzo na hutunza uzito uliokusudiwa kwa muda mrefu. Pia hupunguza mafuta ya mwilini, huongeza ufanisi wa moyo, hupunguza tatizo la shinikizo la damu (hypertension), na kuweka sukari katika kiwango kinachohitajika mwilini.

Kama hujazoea kufanya mazoezi ni vizuri uanze taratibu na ujiwekee lengo kwa kufanya mazoezi kwa muda wa nusu saa kila siku, siku tano kwa wiki,(dakika 30 kila siku kwa siku tano kwa wiki). Mazoezi mazuri ni kama kuogelea, kuendesha baiskeli, kutembea, kunyanyua vitu vizito (visiwe vyenye uzito mkubwa), mazoezi ya viungo na kadhalika.


Kama mtu ni mnene sana basi ni bora kuzungumza na daktari wako kabla ya kuanza mazoezi mapya. Baada ya kuanza mazoezi kwa mara ya kwanza, mwili utakuwa na maumivu, hii ni kawaida lakini kama mtu atapata maumivu zaidi ya masaa 2 baada ya kufanya mazoezi ni vizuri kumuona daktari.
 
Angalia kama kuna kitu kimekubadilisha, Umejifunza nini kutokana na hilo kosa, Utaboreshaje maisha yako. Sema mwenyewe kama hivi kila siku , Nimejisamehe mwenyewe. Kwa makosa yangu na kujiruhusu kusonga mbele, Yaliopita yamepita , Natazama yajayo.

Baada ya kuwasiliana peke yako na msamaha, unaweza kuwasiliana hata na mwingine ambaye umemkosea kwa urahisi, kwa kuelewa na kuomba msamaha wa kweli. Utaweza kutafuta njia nzuri ya kufanya kitu fulani kwa mtu ambaye umemkosea kwa kumsaidia ili aweze kuboresha maisha yake. Jionyeshe mwenyewe na Ulimwengu ambao umejifunza kutokana na makosa.
 
Back
Top Bottom