Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unapokuwa hujisikii vizuri , Tambua maumivu yako kwa njia ya ufahamu kwa kuelewa zaidi kuhusu wewe mwenyewe.Shughulikia tatizo, Usikubali kushindwa na hali hio., lakini jifunze kuwa bora na kujiandaa kwa ajili ya kazi nyingine na ushukuru kwa hio iliopita. Haijalishi ulifanya kazi kwa kiasi gani. tambua kuwa hakuna kilicho na ahadi ya kudumu.
 
Nilipofungua ukurasa wangu wa facebook miezi kadhaa iliopita. Hiki ndicho nilichokiona. Picha ya msichana ambaye amevaa miwani ya rangi nyeusi, Anatabasamu, anaonyesha meno yake meupe, anaonekana yuko huru, anaonekana mwenye furaha. nilitingisha kichwa changu na kuingalia picha hio kila kona . lakini bado anaonekana na furaha.
 
Niliendelea kuangalia ukurasa wake na kuona siku ya kuzaliwa kwake alivyokuwa anafurahia kumbukumbu hio na marafiki zake…amezungukwa na zawadi , anapigwa picha nyingi, anacheka, akiwakumbatia rafiki zake na mengine mengi yaliendelea…
 
Nilichokizoea ni kuona picha za watu wenye huzuni huwa wamelala kitandani , hawawezi kuamka , nywele chafu, anaonekana kama hajaona mwanga hata kidogo, macho yamejaa, nguo alizovaa hazieleweki, yuko kwenye chumba cha giza, na machozi yanatiririka mashavuni. Nafikiri umepata picha hio.
 
Fikiria picha nyingine ya kuudhi, kijana wa kike ambaye anapost picha zake nyingi kwenye instagram. Ndio. yule ambaye anakulazimisha kununua nguo zenye majina, au kunywa kinyaji chenye jina, kahawa yenye jina. Hebu piga picha hio, mfanyakazi mwenzako au mwalimu wako, au rafiki yako, au best friend wako.
 
Back
Top Bottom