Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2017-11-05-14-24-25.png
 
Kama kuna sehemu ambayo Apple wamewashinda Google katika eneo la simu basi ni jinsi ambavyo wanasimamia programu endeshaji ya iOS kuhakikisha inafanya kazi kwa ufanisi mkubwa ukilinganisha na hali inayojitokeza kwa Android. Una uhakika wa kutumia simu yako kwa ufanisi mzuri tuu kwa miaka kadhaa tokea uinunue.
 
Kupata masasisho mapya (Updates)

Makampuni ya utengenezaji simu yanayotumia Android huwa yanachukua toleo zuri lisilo na makorokocho mengi kutoka Google na kisha kila kampuni huingiza apps na kufanya maboresho mengine kwa Android kiasi cha kuathiri ufanisi na ubora wake.
 
Muonekano rahisi kwa utumiaji

Kwa watu ambao si watundu sana na wanapenda simu janja (smartphone) huku utumiaji wao mkuu ukiwa ni kupiga na kupokea simu, kupiga picha na kutumia ujumbe mfupi basi iPhone zina muonekano rafiki zaidi kwao. Ni rahisi kuitumia haraka kwa maeneo hayo, haiitaji ujuzi na utundu sana.
 
>Apps



Ni rahisi zaidi kuwa na uhakika wa apps salama na zenye kufuata sheria kali ya kiwango cha ubora katika soko la apps la Appstore. Soko la apps la Google limejikuta mara kwa mara katika matatizo ya kuruhusu apps zenye ubora wa hali ya chini na ata kuathiri utendaji kazi wa simu zinapotumika.
 
Ubora wa Kamera na simu zenyewe

Apple wanajitahidi sana kuhakikisha simu zao zinakuja na kiwango cha ubora wa juu katika eneo la kamera na ata simu zenyewe kwa ujumla wake. Ni makampuni machache yanayotengeneza simu zinazotumia Android yanayojitahidi kufikia na kuvipita viwango vya ubora huo.
 
Back
Top Bottom