Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

9d769d75f8a6b044cba7c016e560b49d.jpg
 
MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU DAWA, MADUKA YA DAWA MUHIMU NA FAMASI

Hello rafiki! Leo napenda nikujuze mambo 10 kuhusu dawa, maduka ya dawa muhimu na famasi. Utajifunza mambo mengi hapa na mawazo yako yatabadilika. Utapata faida nyingi sana kiafya, kiuchumi na kimaisha kwa ujumla.
 
Dawa ni bidhaa zinazosimamiwa na sheria kali sana
Kuanzia uzalishwaji wake, usambazwaji, uuzwaji, matumizi mpaka uteketezwaji wa dawa zilizoharibika vyote viko chini ya sheria. Dawa zote zilizofuata utaratibu huo huwa ni salama kwa kiasi kikubwa sana.

Sheria hizo zimeweka matakwa makubwa kabla ya kuanza biashara hii, ndio maana huwa na kazi na hata kuchukua mitaji mikubwa katika kuanzishwa kwake. Hii imesaidia sana katika kuhakikisha ubora na usalama wa dawa na afya za watu kwa ujumla
 
Dawa ni sumu kama sumu zingine

Ndio. Ndio maana hata leseni zake huzisema “PART II POISONS” , yaani “SUMU DARAJA LA PILI”.

Hapa maana yake kuu ni moja, dawa zinaweza kuudhuru mwili, mtoto aliyepo tumboni, zinaweza kuua nk endapo zitatumika vibaya. Tunajua kwamba kuna dawa zina uwezo wa kuharibu maini, figo, masikio, ubongo, mimba, kusababisha ulemavu, mfumo wa fahamu na viungo vingine vya mwili.
 
Pointi ya kuzingatia hapa ni kwamba dawa zote zitumike vizuri. Zitumike kama zilivyolengwa na watengenezaji na kuelekezwa na daktari na mfamasia. Matumizi mabaya ya dawa ni hatari sana kwa afya zetu. Kuacha kumeza dawa baadhi ya nyakati, kutomaliza dozi, kumeza dawa zaidi ya ulivyoelekezwa, kumeza dawa ambazo haziruhusiwi kwako (mjamzito, mtoto, una magonjwa yanayoingiliana na dawa nk) hukuweka katika hatari ya kudhurika, kutopona vizuri, kuharibu ufanisi wa dawa, kuzidiwa na hata kufa.
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya duka la dawa muhimu na famasi

Maduka ya dawa muhimu yameruhusiwa na baraza la famasi Tanzania kwa lengo kuu la kurahisisha upatikanaji wa dawa kwa maeneo ambayo yako pembeni mwa mji na vijijini. Hayaruhusiwi kuwepo mjini. Haya unayoyaona maeneo ya mjini yote yanaibia tu na hufanya kwa kuvizia. Maduka ya dawa muhimu yanaruhusiwa kuuza baadhi ya dawa tu, na si dawa zote
 
Back
Top Bottom