Nini cha kutarajia.
Saratani aina ya Anaplastic carcinoma ina matokeo mabaya zaidi kuliko aina zote zilizobaki, na mara nyingi mgonjwa hufariki hata baada ya matibabu ya uhakika ya muda mrefu. Follicular carcinomas pamoja na kuwa na tabia ya kusambaa kwa kasi.
kwenye maeneo mengine ya mwili huwa na matokeo mazuri ikitibiwa. Matokeo ya wagonjwa wenye aina ya medullary carcinoma yanatofautiana kati ya mgonjwa na mgonjwa, ambapo wanawake wenye umri chini ya miaka 40 wameonekana kuwa na matokeo mazuri zaidi baada ya tiba kuliko walio na zaidi ya umri huo. Aidha wagonjwa wengi wenye Papillary carcinomas hupona kabisa na kuendelea na maisha yao ya kawaida.
Jambo la kukumbuka ni kuwa, mara baada ya tiba, mgonjwa anapaswa kuendelea kutumia vidonge vya kurejesha homoni za thyroid kila siku za maisha yake.