Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Antoine Griezmann anaonekana yuko mbioni kutua Barcelona dirisha la kiangazi baada ya klabu hiyo ya Catalan kupiga hatua nzuri ya mazungumzo na Atletico Madrid.

Mfaransa huyo anayewaniwa na Manchester United, moyo wake unaitaka safari ya kuondoka Atletico baada ya uhamisho wake kwenda Old Trafford kiangazi kilichopita kushindikana.

Kwa mujibu wa gazeti la Mundo Deportivo la Hispania, Barcelona sasa ipo kwenye nafasi nzuri ya kumsajili mshambuliaji huyo na kwamba kimsingi makubaliano ya awali yameshaafikiwa.
 
STRAIKA wa Manchester United, Romelu Lukaku, amesisitiza kuwa kurejea kwa staa mwenzake, Zlatan Ibrahimovic, kutawaongezea nguvu katika mbio za kuwania ubingwa Ligi Kuu England.

Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 36, hajacheza hata dakika moja kwenye kikosi hicho cha Mashetani Wekundu tangu asaini mkataba mpya majira ya joto, kwani bado anauguza majeraha yake ya goti aliyoyapata Aprili mwaka huu.
 
Ibrahimovic ambaye aliongoza kwenye orodha ya mabao Man United katika kampeni yake ya kwanza Old Trafford, anatarajiwa kurudi dimbani kabla ya mwisho wa mwaka.

Alipoulizwa kuhusu mchango anaoutarajia kutoka kwa mchezaji mwenzake huyo, Lukaku aliiambia Sky Sport News: "Kurudi kwa Ibrahimovic kutatusaidia kuifukuzia Manchester City.

"Timu kama yetu ni ngumu sana kwa timu pinzani. Inanihamasisha kwa kweli, kwa sababu ni mchezaji mwingine bora sana atakayeongeza nguvu kikosini mwetu."
 
Danny Welbeck amepigwa picha akiwa mazoezini akielekea kupona maumivu yake ya nyama za paja kuelekea mchezo wao wa watani wa jadi dhidi ya Tottenham Jumamosi hii.

Huku Olivier Giroud akiwa mashakani, Welbeck, 26 anaweza akawa miongoni mwa wa wachezaji wa Arsenal watakaoivaa Tottenham kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu utakaopigwa dimba la Emirates.
 
48536b3d08303a33819ba61ab31cb958.jpg
 
Back
Top Bottom