Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nimekupata vizuri sana
 
Baadhi ya wenye nyumba bado wanaendelea kuchukua kodi za wapangaji ila kwa sasa tumetoa agizo kwa viongozi wa serikali za mitaa kuwa mikataba yote ya upangishaji vyumba au nyumba ipitie huko ili tuwaonyeshe wananchi maeneo sahihi ya kupanga,” aliongeza.
 
Bomoabomoa yazua taharuki Dodoma

Mjini Dodoma, Kampuni ya Miliki ya Raslimali za Reli (Rahco) imezua taharuki baada ya kutangaza bomoabomoa kwa wafanyabiashara zaidi ya 1,000 waliojenga majengo na vibanda vya biashara katika hifadhi ya reli.
 
Juzi jioni, gari la matangazo lilipita likiwatangazia wafanyabiashara hao kuwa Rahco ingeendesha bomoabomoa kuanzia saa 12:00 jana asubuhi.
 
Wafanyabiashara wanaotakiwa kubomoa majengo yao ni wale waliojenga kandokando ya stendi ya daladala ya Jamatini, soko la Sarafina, kituo cha mafuta, mama lishe na vibanda vya kukatia tiketi za mabasi yaendayo mikoani.
 
Waliojenga eneo la hifadhi ya reli, wanaofanya biashara eneo la hifadhi ya reli waondoke kabla ya kesho (jana) sasa 12.00 asubuhi. Ikifika asubuhi hujaondoka hutaruhusiwa kuchukua kitu chochote ndani,” alisema.
 
Kuna kaukweli hapo
 
Hata hivyo, baada ya matangazo hayo wafanyabiashara walijikusanya na kuwaita viongozi mbalimbali wa mkoa akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge.
 
Wakizungumza katika mkutano huo, wafanyabiashara hao walisema wako tayari kuondoka kwenye maeneo hayo kwa ajili ya kupisha ujenzi huo, lakini wakaomba kupatiwa maeneo mbadala na muda wa kuondoka katika hilo.
 
Mmoja wa wafanyabiashara hao, Sakina Said alisema hawapingani na kauli ya Serikali juu ya kupisha maeneo hayo kwa ajili ya maendeleo ya Taifa bali wanaomba kupatiwa eneo jingine na muda wa kujiandaa kuondoka.
 
Mkuu wa mkoa tunaiheshimu na kuitii Serikali yetu tukufu chini ya uongozi wa jemedari mkuu Rais Dk John Magufuli, tunachokuuomba tupatiwe muda na tuonyeshwe maeneo ambayo tutafanyia biashara zetu,” alisema.
 
Mfanyabiashara mwingine Jonath Jonathan alisema wengi wa wafanyabiashara wamechukua mikopo benki ambayo wanatakiwa kurejesha kwa wakati na kuomba Serikali kuwafikiria kuwapa muda na kuwatafutia eneo mbadala.
 
Akizungumza katika hadhara hiyo, Dk Mahenge aliwataka wafanyabiashara hao kutii amri ya kuondoka kwenye maeneo hayo ili kupisha ujenzi wa reli mpya ya kisasa.
 
Alisema mkandarasi ameshawekeana mkataba na Serikali na kwamba kazi ya ujenzi wa reli hiyo inatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…