Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nyota wa Manchester United, Romelu Lukaku na mwenzake wa Manchester City, Vincent Kompany ambao ni raia wa Belgium, hawakausita kusalimiana licha ya timu zao kufanyiana ubabe uwanjani.

Mechi hiyo iliisha kwa Manchester City kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya kikosi cha Jose Mourinho, lakini matokeo ya uwanjani hayakuwa kikwao kwa mastaa hao kupeana mikono.

Licha ya Mourinho kuonekana akilalamika kwenye mchezo huo kutokana na kutoridhisha na maamuzi uwanjani, lakini Lukaku hakuonyesha tofauti yoyote kwa mchezaji mwenzake wa Belgium, Kompany baada ya mpira kumalizika.
 
Kocha wa zamani wa Manchester United, Louis van Gaal amemshambulia Jose Mourinho kutokana na kukiongoza kikosi chake juzi Jumapili jambo lililowafanya waonyeshe soka la kichovu na kufungwa na Manchester City.

Kocha huyo mwenye mika 66 amemvaa bosi huyo wa Manchester United kwa madai kwamba mtindo wake wa kucheza ndio umemponza.

Van Gaan ameweka wazi kwamba soka la kocha huyo ni kwamba linaboa uwanjani jambo ambalo liliwapa wapinzani wao kuwaadhibu kwa mabao 2-1.

Pia hakusita kumpa sifa kocha Pep Guardiola pamoja na safu yao ya ushambuliaji ambayo imekuwa makini kuzuia maadui.
 
Nyota wa Liverpool Mohamed Salah ameshinda tuzo ya BBC ya Mchezaji Bora wa Afrika 2017
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ameondoka na tuzo hiyo kutokana na kiwango chake hatari mbele ya goli - akitupia mabao 19 katika michuano yote akiwa na Reds msimu huu.
Salah, ambaye alisaini mkataba kujiunga na klabu hiyo ya Merseyside akitokea Roma kwa kiasi cha takribani paundi milioni 34, alikuwa na mchango mkubwa pia kwa Misri kufuzu Kombe la Dunia 2018 litakalofanyika Urusi.
 
Nina furaha sana kupata tuzo hii, ni hisia za kipekee sana kwangu," mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea aliambia BBC Sport. "Ningependa kumshukuru kila mmoja; wachezaji wenzangu na watu ninaofanya nao kazi.
"Nina furaha sana hapa klabuni, nimekuwa na mwanzo mzuri sana hapa. Pia meneja [bosi wa Liverpool Jurgen Klopp] amenisaidia kutulia kwenye timu.
"Msimu uliopita ulikuwa mzuri kwangu nikiwa Roma, kwa hiyo nataka kuwashukuru wachezaji wenzangu hapa na kwenye timu ya taifa. Watu ninaofanya nao kazi wana weledi sana na nafurahi kuwa nao. Ningependa kushinda tena mwaka unaofuata."
 
Nina furaha sana kupata tuzo hii, ni hisia za kipekee sana kwangu," mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea aliambia BBC Sport. "Ningependa kumshukuru kila mmoja; wachezaji wenzangu na watu ninaofanya nao kazi.
"Nina furaha sana hapa klabuni, nimekuwa na mwanzo mzuri sana hapa. Pia meneja [bosi wa Liverpool Jurgen Klopp] amenisaidia kutulia kwenye timu.
"Msimu uliopita ulikuwa mzuri kwangu nikiwa Roma, kwa hiyo nataka kuwashukuru wachezaji wenzangu hapa na kwenye timu ya taifa. Watu ninaofanya nao kazi wana weledi sana na nafurahi kuwa nao. Ningependa kushinda tena mwaka unaofuata."
 
Sadio Mane anayecheza kikosi kimoja na Salah Liverpool naye alikuwa kwenye kinyang'anyiro cha tuzo hiyo, sambamba na Naby Keita wa RB Leipzig, Pierre-Emeric Aubameyang na Victor Moses wa Chelsea.
Mshindi ndiye kinara wa mabao wa Ligi Kuu Uingereza kwa sasa akiwa na mabao 13.
 
Bakayoko ameshindwa kuonyesha kile kilichotarajiwa kutoka kwake ingawa mchango wake kwenye timu bado ni muhimu, na Kante amemba Mfaransa huyo asaidiwe
Kiungo wa Chelsea N'Golo Kante amesema kuwa timu yake ina jukumu la kumsaidia mchezaji mwenzao Tiemoue Bakayoko anapoendelea kuzoea maisha ya Ligi Kuu Uingereza.
Mfaransa Bakayoko, anahangaika kuonyesha tofauti Chelsea tangu atue London akitokea Monaco kwa £40m, alitolewa kipindi cha pili klabu hiyo ikifungwa 1-0 na West Ham Jumamosi.
 
Kante, ambaye ameshinda tuzo ya PFA ya mchezaji bora wa mwaka msimu uliopita, ameitaka klabu kumsaidia Mfaransa mwenzake.
"[Bakayoko] anafanya mazoezi kwa bidii na anajitoa kikamilifu. Tunapaswa kumsaidia acheze katika ubora wake," Kante alikiambia Evening Standard.
"Je! Timu inawajibika kuweza kumsaidia kucheza katika kiwango bora? Naam. Lakini si Tiemoue pekee, kwa kila mtu. Ni budi tushirikiane kwa ajili ya mafanikio ya timu, kwa kujaribu kushinda mechi. Hilo ndilo tunalofanyia mazoezi.
 
Kama anahitaji ushauri, Naweza kumshauri. Lakini kama ilivyo kwenye kila klabu - jaribu kufanya mazoezi, elewa anachotaka kocha na ujitume dimbani. Ipo hivyo kila mahali."
Chelsea wataikabili Huddersfield Town Jumanne jioni wakitaka kurejea kwenye njia za ushindi baada ya kuangukia pua wikiendi.
 
Muitaliano huyo amesisitiza kuwa Ligi ya Uingereza ndiyo kipaumbele chake lakini amekiri kuwa Barcelona ni mpinzani mgumu anayehitaji nguvu kumfunga
Bosi wa Chelsea Antonio Conte amedai kuwa timu yake italazimika "kucheza kwa 120%" ili kuweza kuing'oa Barcelona Ligi ya Mabingwa hatua ya 16-Bora.
Blues wamepangwa kucheza dhidi ya miamba wa Hispania katika droo iliyofanyika Jumatatu, mechi ya kwanza ikitarajiwa kufanyika Stamford Bridge Februari 20.
 
Conte amesisitiza kuwa nguvu zake ameelekeza kwenye Ligi Kuu Uingereza, lakini Muitaliano huyo amekiri kuwa timu yake imepangwa dhidi ya mpinzani mgumu ambaye ni kinara wa La Liga.
"Ni lazima tuwe tayari kucheza nyumbani. Hakuna faida ya kuanzia nyumbani. Dhidi ya Barcelona ni lazima ucheze kwa 120%," Conte aliwaambia waandishi.
 
Kipaumbele chetu ni ligi na kubaki juu kupigania kutinga nafasi ya nne - kwa sasa. Utakapofika muda wa kuikabili Barcelona tutaanza kuifikiria mechi hiyo."
Chelsea wanataka kurejea kwenye njia za ushindi baada ya kuchezea kichapo cha 1-0 kutoka kwa West Ham United Ligi Kuu Uingereza watakapoitembelea Huddersfield Town Jumanne usiku.
 
Hongereni Wakenya. Mungu Amewavusha salama. Safi sana !!!
e927427ea0a22c57e88524e2ca8df0bf.jpg
Odinga anajiapisha lini?
 
Back
Top Bottom