Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Soko la mboga Tandika
8fd0768f5427898216d0ae881dff564e.jpg
 
Hofu iliyopitiliza (GAD) husababishwa na nini?
Chanzo halisi cha matatizo ya kuwa na hofu kupita kiasi hakifahamiki. Hata hivyo kuna baadhi ya vitu ambavyo vimegundulika kuwa vinachangia sana kuwepo kwa tatizo hili miongoni mwa watu.
 
Vitu/mambo hayo ni pamoja na:
• Nasaba (genetics): baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa nasaba ina nafasi kubwa ya kumfanya mtu wa familia yenye matatizo ya hofu iliyopitiliza naye kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata haya. Hii inaamnisha kwamba, hofu iliyopitiliza inaweza kurithiwa miongoni mwa wanafamilia.
 
Kazi ya kemikali hizi ni kupitisha taarifa na ujumbe mbalimbali kutoka seli moja ya neva mpaka seli nyingine. Iwapo kemikali hizi zitakuwa katika kiwango kisicho sahihi (ama kupungua au kuongezeka) taarifa hazitaweza kusafirishwa kati ya seli za neva na hatimaye hazitaweza kuufikia ubongo inavyotakiwa.
 
Sababu za kimazingira: matukio kama vile ajali, kuumia au matukio yenye msongo mkubwa kama vile kunyanyaswa kwa namna yeyote ile, kufiwa na mtu unayempenda, talaka, kubadilisha kazi au kuachishwa/kufukuzwa kazi, kubadilisha shule au kufukuzwa/kuacha shule nayo pia yanaweza kusababisha kuwa na hali ya hofu iliyopitiliza.
 
Hofu (GAD) pia huwa mbaya zaidi kipindi ambapo muhusika huwa katika hali ya msongo mkubwa wa kimaisha (stress). Aidha matumizi ya vitu vyenye kulevya kama pombe (alcohol), sigara (nicotine) au hata kahawa nayo pia yanaweza kuongeza ukubwa wa tatizo hili. Kadhalika, watu waliokuwa watumiaji wakubwa wa vitu hivyo kisha wakaacha ghafla, nao wapo katika hatari kubwa ya kukumbwa na tatizo hili.
 
Ukubwa wa tatizo
Bahati mbaya, takwimu za ukubwa wa tatizo nchini Tanzania hazikuweza kupatikana. Hata hivyo, inakadiriwa kuwa takribani watu wazima milioni 4 mpaka 5 huko nchini Marekani hukumbwa na tatizo hili kila mwaka.
Kwa kawaida, wanawake huathiriwa zaidi kuliko wanaume. Aidha hofu iliyopitiliza mara nyingi huanza kipindi cha utoto au utoto kabla ya ujana ingawa pia inaweza kutokea wakati wa utu uzima.
 
Vipimo na uchunguzi
Iwapo mgonjwa ana dalili za hofu iliyopitiliza, kwanza daktari atataka kufahamu historia yake kwa kumuuliza maswali juu ya maisha yake na dalili zinazomsumbua kabla ya kumfanyia uchunguzi wa mwili mzima ili kufahamu kama hana tatizo jingine la mwili linaweza kumletea dalili kama hizo.
 
Kuweza kutambua kama mgonjwa ana tatizo hili, daktari atatilia mkazo kwenye ukubwa wa tatizo lenyewe, muda tangu dalili zilipoanza kujitokeza, na iwapo tatizo hili linamfanya mgonjwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kila siku.
 
Back
Top Bottom