Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Alipotafutwa msemaji wa wizara hiyo, Benny Mwaipaja kwa kutumiwa ujumbe wa baruapepe tangu Novemba 16, 2017 ili kufahamu namna fedha za akaunti hiyo zinavyotumika alitaka apewe muda, lakini pamoja na kukumbushwa hakuweza kutoa majibu.
 
Gazeti hili pia lilitaka kufahamu kiasi kilichopatikana walau ndani ya miaka mitatu iliyopita na kinachotumika kila mwaka kutoka kwenye akaunti hiyo kwa walau miaka 10 kama takwimu husika zipo, lakini baruapepe za kuulizia suala hilo na kukumbushia hazikupata majibu.
 
Licha ya usalama wa fedha za wateja wa M-Pesa ambao ni zaidi ya milioni 7.7 kati ya watumiaji wote wa huduma za fedha kwa simu ya mkononi ambao takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) zinaonyesha ni milioni 20.3, Ferrao alieleza mafanikio na changamoto za kampuni hiyo kwa nusu mwaka.
 
Kwa miezi sita kuanzia Aprili mpaka Septemba 2017, kampuni hiyo iliongeza mapato yake na kupata faida ya asilimia 3.9 hivyo kuwa na uhakika wa kutengeneza faida ya Sh96 bilioni zilizokusudiwa mwishoni mwa mwaka.
 
Licha ya changamoto zilizopo sokoni, alisema kampuni hiyo yenye wateja wengi zaidi wa mawasiliano nchini imeweka mikakati ya kukabiliana nazo ili kutimiza malengo iliyonayo ikiwa ni pamoja na kutoa gawio kwa wanahisa wake. Waraka wa matarajio wa Vodacom unaonyesha nusu ya faida yake inapaswa kutolewa gawio kila mwaka.
 
Soko la data linakua kila siku lakini changamoto iliyopo ni bei kubwa ya simu za kisasa inayotokana na kodi iliyowekwa. Serikali ikiiondoa, Watanzania wengi watamiliki simu hizi na kuongeza matumizi ya data hivyo mapato ya kampuni za simu,” alisema Ferrao.
 
Meneja wa viranja wa Ligi ya Premia Manchester City Pep Guardiola amesema mpangilio wa mechi nyingi msimu wa sikukuu umekuwa "janga" kwa wachezaji.
City, ambao wamo alama 12 mbele ligini, wakiwa na mechi moja hawajacheza, watakutana na Watford Jumanne, ambayo itakuwa mechi yao ya nne katika siku 11 msimu wa Krismasi na Mwaka Mpya.
Wachezaji wao muhimu Gabriel Jesus na Kevin de Bruyne waliumia wakati wa mechi dhidi ya Crystal Palace Jumapili.
Mhispania huyo alisema: "Iwapo utaniambia kwamba kiufundi, kimwili inawafaa wachezaji: la hasha, ni janga."
Jesus aliandika Jumatatu kwamba anaona heri kidogo kwamba hatahitaji kufanyiwa upasuaji.
 
Mkimbio wa City wa kushinda mechi 18 mtawalia ulifikishwa kikomo walipotoka sare Selhurst Park ikiwa ni mara yao ya kwanza kushindwa kufunga kwenye mechi ligini msimu huu.
Ikizingatiwa kwamba amekuwa mkufunzi Uhispania na Ujerumani ambapo kipindi hicho timu hupumzika, Guardiola alisema imemlazimu kuzoea utamaduni wa Uingereza.
 
Guardiola amewahimiza waamuzi "kuwalinda" wachezaji dhidi ya kukabwa vikali.

Alikuwa amedokeza kwamba anatarajia Jesus atakuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja au zaidi kidogo.
Ubaya wa jeraha la De Bruyne bado haujabainika.
 
Jose Mourinho amemshutumu nyota wa zamani wa Manchester United Paul Scholes baada yake kumkosoa mara kwa mara kiungo wa kati kutoka Ufaransa Paul Pogba.
Akizungumza baada ya sare ya 0-0 kati ya klabu hiyo na Southampton Jumamosi, Scholes alisema: "Haonekani kama mchezaji ambaye atakusaidia kushinda mechi - mchezaji kama huyo ndiye unafaa kutoa £90m mfukoni kwa sababu yake."
Baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Everton Jumatatu, Mourinho alisema: "Jambo pekee analofanya Scholes ni kukosoa tu.
"Scholes atakumbukwa kwenye historia kama mchezaji stadi. Si kama mchambuzi mahiri wa soka.
 
Tamko la Scholes mwishoni mwa wiki alilitoa baada ya United kutoka sare mechi ya tatu mtawalia.
Mchezaji huyo wa zamani wa England ambaye sasa ana miaka 43 amekuwa akifanya kazi kama mchambuzi katika runinga ya BT Sport na alikosoa mtazamo wa Pogba na kudokeza kwamba huenda pia hayuko sawa kimwili kucheza.
 
'Anazurura' tu wakati wa mechi," alisema Scholes.
"Pogba haonekani kuwa sawa kucheza, nashangaa iwapo anafanya mazoezi vyema.
"Hakuna yeyote England anafaa kuwa akifika karibu naye, lakini anatakiwa kufanya majukumu ambayo hapendezwi nayo.
"Inabidi useme kwamba meneja anafaa kulaumiwa kwa hilo."
 
Pogba, 24, alicheza zaidi safu ya mashambulizi dhidi ya Everton zaidi ya alivyocheza dhidi ya Southampton, na alisaidia mabao yaliyofungwa na Anthony Martial na Jesse Lingard waliposhinda 2-0.
Mourinho alisema: "Sifikiri yeye (Shcoles) huwa anatoa maoni. Yeye hukosoa - ambalo ni jambo tofauti.
"Si kila mtu anaweza kuwa stadi kama alivyokuwa. Alipokuwa mchezaji alikuwa hodari ajabu, lakini haina maana kwamba sote twafaa kuwa kama yeye.
"Wakati mwingine Pogba hucheza vyema, wakati mwingine hucheza vyema na wakati mwingine huwa hachezi vyema. Pogba hutia bidii kila wakati.
 
Si kosa lake Paul kwamba ameunda pesa nyingi zaidi ya Paul Scholes. Si kosa la Paul Pogba, ni vile tu soka ilivyo."
Mourinho aliongeza pia kwamba iwapo Scholes atakuwa meneja siku moja, "ningependa sana awe na ufanisi angalau 25% ya ufanisi wangu."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…