Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Najua kuna baadhi ya imani zisizo rasmi ambazo hujaribu kulielezea suala hili. Mfano; Ukiona bundi asubuhi au ukipishana na vyoka njiani basi kuna walakini na siku yako hiyo. Wapo wengine hasa wazungu ambao husema : “ameamkia upande mbaya wa kitanda” sina uhakika kama kuna upande mbaya na mzuri wa kitanda.
 
Je, umeshawahi kufanya kitu fulani na baadaye ukajutia kukifanya kitu hicho?
Umeshawahi kufanya kitu na ukajihisi kushindwa au kuaibika?
Umeshawahi kudhamiria kuingia kwenye uhusinao kwa matumaini yote na mara ukaona kila kitu kina kuwa ndivyo sivyo?
Au umeshapitia matatizo fulani ya mwili, kama vile Ugonjwa, ukilema na ukaona labda ndiyo chanzo cha ugumu wa maisha yako?
 
Mambo ya kuzingatia:
Jikubali kama mwanadamu wa kawaida na kwamba haistajabishi kushindwa
Yamkini unakata tamaa maana umezungumza na watu wanaoshinda na kufanikiwa tu, angalia upande wa pili, zungumza pia na waliowahi kushindwa.
 
Haijalishi ni muda gani, ni kiasi gani, ni ukubwa gani, ni uzito kiasi gani, wa magumu uliyopitia ninachojua ni kwamba inawezekana mimi na wewe kunyanyuka tena toka kushindwa kwetu, ndoto zetu zaweza kuwa kweli tena. Hii inategemea na kiasi cha uvumilivu wako.
 
Tatizo siyo kushindwa. Kushindwa kwa ukweli ni kule kushidwa kunyanyuka tena mara baada ya kushindwa mara ya kwanza
Angalia mchezo wa ngumi, haijalishi mtu anapigwa na kuanguka mara nyingi kiasi gani, lakini pale anaposhindwa kunyanyuka ndiyo refa hutangaza “KNOCK OUT” yaani ameshindwa kabisa.
 
-1790170957-1525563378.jpg
 
Ili kuweza kunyanyuka tena;
Jikubali kama mwanadamu wa kawaida tambua kushindwa kupo na ni moja ya matukio ya maisha yetu.
Unapoanguka chini, jitahidi usibaki chini. (Tofautisha kuanguka kwa mtoto na mtu mzima) fahamu kushindwa kwa kweli ni kule kushindwa kunyanyuka mara baada ya kuanguka.
 
Tutakushangaa, ukiangushwa na jambo lile lile linalokuangusha mara zote.
Jifunze kutumainia katika imani uliyonayo. Imani ni injini isiyoshindwa. katika suala zima la kushindwa na kuweza. Imani huwa poozeo kwa maumivu tunayoyapitia.
 
Back
Top Bottom