Wenger amekusanya pesa katika madirisha haya mawili ya uhamisho baada ya kuwauza baadhi ya mastaa wake kama vile Gabriel, Alex Oxlade-Chamberlain, Theo Walcott, Francis Coquelin, Alexis Sanchez huku sasa akitazamiwa kumuuza Giroud.
Arsenal pia imeendeleza mbio zake za kumchukua beki wa kati wa West Brom, Jonny Evans na kwa sasa haina upinzani katika mchakato wa kuisaka saini ya beki huyo wa zamani wa Manchester United kwa sababu wapinzani wao katika saini hiyo Manchester City wanakaribia kumnasa beki wa Athletic Bilbao, Aymeric Laporte.