Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Masoko wa TBL - Afrika Mashariki, Thomas Kemphuis alisema, baada ya uchunguzi wa kina kampuni hiyo imejiridhisha pasipo na shaka kuwa hakuna tukio la aina hiyo lililotokea na kusisitiza taarifa zake zipo salama huku ikiwataka wanahisa wake, wadau pamoja na umma kwa ujumla kutokuwa na wasiwasi. Akisisitiza nia ya TBL kuendelea kutoa huduma bora, Kemphuis alisema kampuni hiyo inachukulia kwa uzito mkubwa suala la usalama wa mifumo yake na ndiyo sababu ya kufanya uchunguzi wa haraka na wakina mara baada ya kupata taarifa za uvumi juu ya udukuzi