Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Siku zote matokeo ya maamuzi yetu ndio huleta furaha au msongo wa mawazo ndani ya maisha yetu. Watu huamua kuuza viwanja na nyumba zao kwa sababu mbalimbali ambazo huwasukuma kufanya maamuzi hayo, kila mtu huwa na sababu tofauti na mwingine, lakini wengi wao sababu hufanana.
 
Kilichotusukuma tuandika Makala hii ni kuona idadi kubwa ya watu waliouza wana sababu ambazo hazina mashiko mbele ya uso wa dunia ya leo. Binafsi sipendi kuona watu wanapoteza rasilimali zao kwa sababu ambazo hazina tija yeyote.
 
Ingawa wengi wao tumejitahidi kuwabadili mitazamo hasi waliyonayo na kuanza safari mpya yenye matumaini ya ushindi bado naamini wapo wengine wengi kwenye jamii zetu wenye mitazamo hasi kuhusu uwekezaji huu wa ardhi na majengo (Real estate, finance and investment).
 
Zifuatazo ni baadhi ya sababu ambazo hazikubaliki kwenye uwekezaji wa ardhi.

1. Umepata Fursa Ya Kazi Mji Wa Mbali

Hakuna aijuaye kesho, lakini usemi huu usitufanye tukose tumaini la kesho. Katika hali ya kutafuta ni kawaida ya watu kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa sababu mbalimbali za kimaisha. Sababu mojawapo huwa ni kuhamishwa kikazi au kupata fursa mpya ya kiuchumi sehemu nyingine.
 
Jambo hili huwa ni changamoto kwa baadhi ya marafiki zetu, hujikuta wapo njia panda na wasipate maamuzi sahihi. Marafiki zetu hawa wameshindwa kutambua kuwa hali ya maendeleo ya sasa inatulazimisha watu kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine ili kupata rasilimali uchumi na jamii.
 
Jambo kama hili linapotokea kwako usifanye maamuzi dhaifu, hata unapokwenda huwezi jua kuwa utatumia muda gani au utaishi milele pasipo kutokea fursa nyingine sehemu tofauti ya mji huo mpya.
 
2. Familia Imeongezeka Na Unahitaji Nyumba Kubwa Zaidi

Familia nyingi za Kiafrika ikiwemo Tanzania bado tuna utamaduni wa kuishi kindugu, hali hii husababisha mtu anayemiliki uchumi mkubwa tofauti na wengine kulazimika kuwahudumia wale wasio imara kiuchumi
 
Hivyo mwisho wa siku utagundua kuwa nyumba uliyonayo imeshindwa kukidhi mahitaji ya ziada kwa ajili ya ongezeko kubwa la wageni ndani ya familia. Katika hali hii watu wengi huamua kutafuta uwezekano wa kutafuta nyumba iliyo kubwa Zaidi kwa kuwa uwezo huo wanao mikononi mwao.
 
Watu hawa wanasahau kuwa mahitaji ya binadamu hayana ukomo milele yote, wanasahau kuwa hata hiyo nyumba atakayo nunua itawavutia wengine Zaidi, gharama ya kukidhi mahitaji ya makazi hayo mapya itaongezeka maradufu siku za usoni na hali ya uchumi hubadilika wakati wowote.
 
Back
Top Bottom