Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Chotara wale wa nyati na ng’ombe walikuwa na tabia kutoka kila upande, lakini walikuwa wapole na wakali wakichokozwa.
Hata hivyo, wale wenye shamba walimtafuta kijana kwa ajili ya kuwachunga, wanyama wale wakamzowea mno kwa sababu ndiye aliyekuwa akiwakamua pia.
 
Wale wanyama walimtambua yule mchungaji wao tu na ikiwa alitokea mtu mwingine tofauti walikuwa wakali mno kama mbogo mwenyewe alivyo. Kwa hiyo hakuna aliyewasogelea isipokuwa yule kijana ambaye kwao alikuwa rafiki.
Sasa utauliza walimtambuaje kama huyo ndiye yule rafiki yao? Ilikuwa rahisi kwao. Yule kijana alizowea kuvaa fulana nyekundu kila siku, kwa hiyo kama angetokea mtu mwingine katika mavazi tofauti wangebadilika na kuwa wakali.
 
Si wenye shamba au mchungaji yule ambaye alielewa kisa cha wanyama wale kumpenda kijana, sana sana wao waliona kwamba ni bahati tu.
Kwa kuwa hakuna aliyejua siri ya kuzoweana huko, siku moja yule kijana akavaa shati lenye rangi tofauti na ile ambayo wanyama walizowea kumuona nayo.
 
62db7a27768783b95f0add976f219604.jpg
Asee
 
Alipowakaribia walibadilika kwa hasira na kuanza kumshambulia. Kelele zake zilisikiwa na wenye shamba ambao walikimbia kwenda kuangalia kulikoni, wakakuta kijana yuko katika hali mbaya sana maana wale wanyama walikuwa wakimwinua kwa pembe zao na kumtupa chini.
Haikuwa rahisi kumuoka mpaka mmoja wa watoto wa mwenye shamba alipoamua kutumia bunduki kumpiga mmoja, akalala chini puu na kufa.
 
Wale wengine wakakimbia mbali kidogo baada ya kuona mwenzao kaanguka. Wenye shamba wakaenda kumwinua yule kijana, lakini alikuwa ameumia vibaya na kwa bahati mbaya akafariki akiwa njiani kukimbizwa hospitali. Tangu wakati huo wale ndugu wakaacha kuwafuga wanyama wale ingawa walikuwa wanatoa maziwa mengi mno na bora.
 
Somo hapa ni kwamba, wanyama tunaowafuga wanatufahamu, tofauti na sisi tunavyofikiria. Wanajua nani ni rafiki na nani ni adui miongoni mwetu; wanajua nani anawatendea wema na nani anawatesa.
Mnyama ambaye ni rafiki, hata ukimwita kwa jina – kama umempatia – lazima atasimama. Au akikuona atakufuata kwa upendo
 
Kama ni mbwa atakukimbilia na kukurukia akicheza cheza, vivyo hivyo hata kwa wengine.
Ikiwa unawalisha vizuri, lazima wakikuona tu bandani watakukimbilia wakijua umewapelekea chakula.
Zamani nilipokuwa nachunga ng’ombe nakumbuka kulikuwa na ng’ombe wetu mmoja mkorofi ambaye ndiye aliyekuwa akiwaongoza wenzake kokote.
 
Lakini aliisikiliza sauti yangu, kama tulikuwa machungani na nilitaka turudi nyumbani, nilikuwa nikisema “Walema (ndilo jina tulilompa) twende nyumbani!” basi aliongoza njia ya nyumbani na wenzake wakamfuata. Huu ndio urafiki kati ya wanyama na binadamu!
Naam. Sungura ni wanyama wapole na wakimya sana lakini hiyo haimaanishi kwamba ‘hawazungumzi’.
 
Lugha ya mwili ndiyo mawasiliano yao ya msingi (kama ilivyo kwa wanyama wote) lakini pia wanatoa sauti ambayo huwezi kuielewa, ingawa inatafsirika.
Kwa nyongeza tu kama ulikuwa hujui ni kwamba, sungura wanajifunza lugha ya pili na wanaweza kuelewa lugha ya binadamu anapoongea.
 
Tabia yao na mbinu za mawasiliano wamezirithi kutoka vizazi na vizazi katika falme ya wanyama ambao ni wanyama wa kuwindwa, jinsi wanavyoshirikiana na kuhabarishana kama kuna hatarini, na kadhalika.
Kama wanyama wa kuwindwa (prey animals), tabia ya sungura imejikita zaidi kwa kutazama hatari na kutafsiri haraka ili kuchukua hatua kabla wanyama hatari hawajawafikia, au hata binadamu wanaowawinda – kwa wale walio porini.
 
Sungura ni wanyama wanaolinda himaya na wako tayari kujilinda dhidi ya wavamizi. Wanawasiliana kwa namna tofauti kuhusu jinsi gani wanaweza kukabiliana na jambo lolote.
Sungura (hata wakiwa porini) huishi katika makundi na kujenga himaya zao. Wanawasiliana kuhusu nafasi zao kwenye himaya kwa kuendeleza tabia za kudumu.
 
Back
Top Bottom