Tabia yao na mbinu za mawasiliano wamezirithi kutoka vizazi na vizazi katika falme ya wanyama ambao ni wanyama wa kuwindwa, jinsi wanavyoshirikiana na kuhabarishana kama kuna hatarini, na kadhalika.
Kama wanyama wa kuwindwa (prey animals), tabia ya sungura imejikita zaidi kwa kutazama hatari na kutafsiri haraka ili kuchukua hatua kabla wanyama hatari hawajawafikia, au hata binadamu wanaowawinda – kwa wale walio porini.