Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

katika Makala hii tutajifunza nini maana ya kupata usingizi mzuri, pengine yeaweekana unaugua kwa kutojua ni upi usingizi wenye afya, tutaangalia baadhi ya mambo yanayopelekea kukosa usingizi na ushauri sahhi na rahisi wa kufuata ili kurudisha usingizi wako mazuri na ukafurahisa Maisha.
 
Dr Naiman ambaye ni mwanasaikologia kutoka Marekani anasema “usingizi siyo tu ni kitendo cha kutokuamka, hii ni tafsiri isiyo sahihi miongoni mwa watu kwenye dunia yetu kwa sasa. Tunatafsiri usingizi kinyume na mana halisi.
 
Jinsi gani tatizo la kukosa usingizi huanza.

Kukosa usingizi ama kupata usingizi wa shida na kuchelewa kupata usingizi ni moja ya matatizo makubwa yanayosumbua watu kwa kipindi hiki, kila siku tunapokea wagonjwa wengi wanaotafuta ushauri jinsi gani warudishe usingizi ,mnono wa mwanzo ili waweze kufuahia Maisha.ili kufahamu kwanini hupati usingizi basi ni muhimu kujua uhusiano kati ya kiwango cha usingizi na usumbufu/kelele.
 
Usumbufu/kelele: usumbufu/kelele ni kitu chochote ambacho kinaharibu ama kuingiia usingizi. Kama kiwango cha usumbufu/kelele kikiwa kikubwa kuliko uwezo wa kusinzia basi ni wazi kwamba utapata shida kusinzia. Usumbufu/kelele zinaweza kuwa kwenye aina tatu, usumbufu/kelele za kimazingira, usumbufu/kelele za kimwili na usumbufu/kelele za `kiakili.
 
Mchana mwili unakuwa na nguvu na ukiwa na motisha kubwa ili kufanya shuguli zako za kimaendeleo, lakini hali hii inapojitokeza wakati wa usikku basi yatakiwa kutambua kuwa kuna tatizo na tutaita ni usumbufu/kelele. Aina mojawapo ya usumbufu/kelele ambazo huingilia Zaidi usingizi kwa watu wengi ni mfululizo wa fikra mbalimbali ambazo zinakuwa zinazunguka kwenye akili wakati wa usiku na hivo kuingilia upatikanaji wa usingizi mtamu.
 
Kwanini ni muhimu kulala kwenye giza nene (complete darkness)
Uwepo wa mwanga kwenye chumba chako cha kulala kinaingilia uzalishaji wa kichocheo cha melatonini ambacho huusika katika kukufanya usinzie. Kupungua kwa uzalishaji wa homoni ya melatonin huweza kuleta athari kubwa kwa afya ya mtu ukiachilia mbali kuharibu usingizi.
 
Mfano utafiti unasema kuna uhusiano mkubwa kati ya upungufu wa melatonin na kuongezeka kwa hatari ya kuugua saratani ya matiti. Miaka ya nyuma kabla teknologia haijakua mababu zetu walilala masaa 12 wakiwa gizazi kabisa, leo hiii kutokana na uvumbuzi wa umeme na taa, tumejikuta masaa 16 tukiyatumia kwenye mwanga na masaa 6 tu tukitumia kwenye giza na tena pakiwa mwanga hafifu kwa nje ukiendelea kuwaka.
 
Back
Top Bottom