Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Maafisa wa uhamiaji nchini Kenya walimzuilia Bwana Orengo na Bwana Wanjigi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Jumatatu
Jumanne , Bwana Kihalangwa alituma ujumbe wa Twitter kwamba hatimae amri ya mahakama imefika na wawili hao wameruhusiwa kuondoka kuelekea Zimbabwe
 
Broke Nigga
2222705d0950684d521a47bfe16c5426.jpg
 
Bwn. Orengo alipinga ujumbe wa Bwn. Kihalangwa, akisema kuwa maafisa wa uhamiaji walipokea amri ya mahakama Jumatatu usiku.
Na kwamba yeye na Bwn. Wanjigi karibia wanakaribia kuondoka kuelekea Zimbabwe baadae Jumanne.
IKatika wiki za hivi karibuni, serikali ya Kenya imekuwa ikiwakamata viongozi wa upinzani wafuasi wa Bwn. Odinga.
 
Binadamu kwa kawaida huwa macho mchana na usiku hulala, ingawa siku hizi si ajabu kwa wengi kulala mchana na kufanya kazi usiku.
Lakini je, umewahi kujiuliza mwanadamu anaweza kukaa muda gani bila kulala?
Vijana wawili nchini Marekani walijaribu kupima hili.
 
Ilikuwa ni mwishoni mwa mwaka wa 1963 na bendi ya Beach Boys ilikuwa ndiyo inavuma zaidi wakati huo.
Marekani ilikuwa pia imeanza kujiingiza zaidi katika Vita vya Vietnam, na watoto wa shule za upili walikuwa wanajiandaa kwa likizo ya Krismasi pale vijana wawili walipoamua kufanya utafiti ambao ulilivutia taifa.
 
Utafiti huu ulifikia kikomo mnamo 8 Januaru 1964.
Randy Gardner wa miaka 17 alikuwa amefanikiwa kukaa macho bila kulala kwa siku 11 na dakika 25 mfululizo.
Bruce McAllister, mmoja wa wanafunzi wa sekondari walioibuka na wazo hilo, anasema hatua hiyo ilitokana na haja ya kuunda mradi wa kuwasilisha katika maonesho ya sayansi.
 
Baada ya kuunganisha ubunifu wao na 'utukutu' kiasi wa ujana, Bruce na rafiki yake Randy waliamua kujaribu kuvunja rekodi ya dunia ya kukaa muda mrefu bila kulala.
Rekodi hiyo wakati huo ilikuwa inashikiwa na DJ mmoja kutoka Honolulu, Hawaii ambaye alikuwa amekaa saa 260 bila kulala (siku 10 na saa 20).
 
Mpango wa kwanza ulikuwa wa kuchunguza athari za kutolala kwenye uwezo wa kiajabu usioeleweka wa ubongo (ikiwa ni pamoja na nguvu za kiroho)," McAllister anasema.
"Tuligundua kwamba hakukuwa na njia ya kupima hilo na kwa hivyo tuliamua kupima basi athari za ukosefu wa usingizi kwenye uwezo wa mtu kufahamu na kutambua mambo, katika kucheza mpira wa kikapu. Jambo lolote tu ambalo tungeweza."
 
Walirusha sarafu juu kuamua ni nani angekaa bila kulala.
McAllister alifurahia sana aliposhinda kuwa 'mtazamaji'.
Lakini ulimbukeni wao ulijitokeza pale kulipozuka kikwazo cha jinsi yeye mwenyewe angemchunguza mwenzake Randy. Angefanya hivyo vipi bila yeye mwenyewe kulala?
 
Tulikuwa wapumbavu. Wajua, wapumbavu wachanga," anasema "na nilikaa macho nikimfuatilia…na baada ya usiku wa tatu bila kulala, mwenyewe nilishangaa kuzinduka na kujipata nilikuwa nimelala kwa kuinamisha kichwa kwenye ukuta, na nilikuwa naandika maelezo ukutani."
Vijana hao waligundua kwamba walihitaji kumshirikisha mhusika wa tatu.
 
Na hapo ndipo walipomwita rafiki yao Joe Marciano kusaidia katika kuwa 'mtazamaji'.
Muda mfupi baada ya Marciano kujiunga nao, mtafiti kuhusu usingizi kutoka Chuo Kikuu cha Stanford William Dement naye alifika.
Dement kwa sasa ni profesa lakini mwaka 1964 alikuwa tu ndio anaanza kazi yake ya utafiti katika fani ya sayansi ya usingizi, ambayo ilikuwa bado change.
 
Alikuwa amesoma habari kuhusu kisa cha vijana hao wawili katika gazeti moja la San Diego na akaamua mara moja kwamba alitaka kushiriki. Hilo kwa kiasi fulani liliwatuliza roho wazazi wa Randy.
"Wakati huo, pengine nilikuwa mtu pekee duniani aliyekuwa amefanya utafiti halisi kuhusu usingizi," Dement anasema.
 
Back
Top Bottom