Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ni ziwa kubwa la pili duniani kwa wingi wa maji matamu baada ya Ziwa Baikal (Siberia) kwa kuzingatia kiasi cha maji ndani yake na kina (hadi mita 1,470).

Kwa kulinganisha eneo lake (km² 32,893) ni la pili tu baada ya Viktoria Nyanza katika Afrika.

Maji yake hutoka kuelekea mto Kongo ha hatimaye katika Bahari Atlantiki.
 
Jina la ziwa limepokewa na Wazungu wapelelezi wa kwanza kutoka kwa wenyeji wa Ujiji. Henry Morton Stanley aliyetembelea ziwa mnamo mwaka 1876 aliandika ya kwamba watu wa Ujiji hawakuwa na uhakika kuhusu maana ya jina, ila tu ilimaanisha ziwa kubwa[1]. Maana waliita maziwa madogo "Kitanga", na waliita pia "ziwa la Usukuma" yaani Viktoria Nyanza kwa jina hili "Tanganika".
 
Wajiji walimwambia Stanley ya kwamba labda neno "nika" ilitoka kwa aina ya samaki walioitwa vile. Baadaye Stanley alikumbuka neno "nika" katika lugha nyingine za Kiafrika kwa maana ya "tambarare, eneo kubwa bapa" akahisi ya kwamba waliita ziwa kama "tambarare kubwa iliyotanda" [
 
Stanley alishika pia majina ya ziwa kwa makabila mengine- watu wa Marungu walisema "Kimana", wale wa Urungu "Iemba" na Wakawendi "Nsaga" kwa maana "ziwa lenye dhoruba". Alichoshika na watu wa Urungu, yaani "Iemba", inalingana na taarifa ya David Livingstone aliyekuta jina "Liemba" kuwa jina la sehemu ya kusini ya ziwa na jina hili linaendelea kutumiwa kwa meli ya MV Liemba inayosafirisha watu na bidhaa ziwani tangu mwaka 1914.
 
Halijoto ya maji usoni mwa ziwa ni sentigredi 25 na uchungu wake ni pH 8.4 hivi.

Urefu wa ziwa ni kilomita 676 kutoka kaskazini hadi kusini na upana wake ni km 50 kwa wastani. Uso wa maji huwa na eneo la km2 32,900 na urefu wa pwani yake ni km 1,828.
 
Kina kikubwa cha ziwa kimesababisha kuwepo kwa safu za maji zisizochanganya maana maji ya chini hayakorogwi kwa upepo au mikondo na maji ya juu, hivyo maji ya chini hayapokei oksijeni na kuwa na uhai kidogo. Samaki na viumbehai wengi hawawezi kuishi katika maji bila oksijeni.
 
Kubadilika kwa kiasi cha maji Edit
Kutokana na mahali pake katika tropiki kwenye jua kali, Ziwa Tanganyika linapotewa na maji mengi kwa njia ya uvukizaji. Kwa hiyo kiasi cha maji ndani yake inategemeana na kiasi cha maji yanayoingia. Kwa sasa chanzo kikubwa ni maji ya Ziwa Kivu. Imegunduliwa ya kwamba uwiano wa ziwa ulibadilika sana katika historia. [5]
 
Mnamo miaka 200,000 iliyopita uso wa ziwa ulikuwa mita 600 chini ya uwiano wa leo. Wakati wa vipindi vya tabianchi yenye mvua nyingi zaidi uwiano ulipanda juu, na kupungua tena kwenye vipindi vya ukame. Vipindi hivi vya mabadiliko vilidumu mara kwa mara miaka elfu kadhaa.
 
Hali ya sasa imepatikana tangu miaka 12,000. Wakati ule volkeno za Virunga vililipuka na kuziba mto uliowahi kubeba maji ya Ziwa Kivu kuelekea mto Naili na baada ya kufikia uwiano wa leo maji ya Kivu yalianza kutoka upande wa Tanganyika kupitia njia ya Ruzizi.
 
Mabadiliko ya uwiano wa maji kwenye ziwa yalitazamwa pia katika historia ya miaka 200 iliyopita kwa kulinganisha kumbukumbu ya wakazi na taarifa za wapelelezi Wazungu walioandika taarifa juu ya safari zao. Baada ya mwaka 1800 maji yalikuwa chini sana, kabla ya 1900 yalikuwa juu sana, tangu 1900 yalishuka tena. Katika miaka ya 1960 ziwa lilijaa tena likabaki hivi hadi sasa.
 
Ni ziwa kubwa la pili duniani kwa wingi wa maji matamu baada ya Ziwa Baikal (Siberia) kwa kuzingatia kiasi cha maji ndani yake na kina (hadi mita 1,470).

Kwa kulinganisha eneo lake (km² 32,893) ni la pili tu baada ya Viktoria Nyanza katika Afrika.

Maji yake hutoka kuelekea mto Kongo ha hatimaye katika Bahari Atlantiki.
kweli..
 
Back
Top Bottom