Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kutokana na mazingira ya pekee ziwa Tanganyika ni mahali pa kutazama matokeo ya mageuko_ya_spishi. [7]

Cichlidae wa ziwa Tanganyika wanapendwa kama samaki wa mapambo wakinunuliwa na kufugwa na wenye tangisamaki kote duniani.

Ziwani kuna pia spishi nyingi za pekee za konokono na kaa pamoja na crustacea nyingine.
 
Tasnia muhimu katika eneo la ziwa ni uvuvi. Inakadiriwa ya kwamba baina ya 25–40% za protini katika chakula cha milioni 1 ya watu wanaoishi kule ni kutoka samaki wa ziwani[8].

Mwaka 2015 kulikuwa na watu 100,000 hivi waliofanya kazi kuhusiana na uvuvi.
 
Samaki wa ziwani wanauzwa kote Afrika ya Mashariki. Katika miaka ya 1950 uvuvi wa kibiashara ulianzishwa ziwani ukasabisha kupotea kwa samaki: kufikia mwaka 1995 mavuno ya samaki yalipungua hadi tani 180,000. Kampuni nyingi za uvuvi zilizostawi katika miaka ya 1980 ziliporomoka.
 
Usafiri ni mgumu kufikia Ziwa Tanganyika kutoka miji mikuu ya nchi zao.

Kuna njia za reli zinazoishia

Kigoma (Tanzania) kutoka Dar es Salaam, bado kwenye njia ya reli iliyojengwa zamani za ukoloni wa Kijerumani
Kalemie (J.D. Kongo) kutoka Lumbumbashi
Mpulungu (Zambia) - hakuna reli bado, ila kuna mipango ya kujenga njia hadi hapa hadi njia kuu ya TAZARA
 
Huduma iliyopo hadi sasa ni ngumu na hali za njia za reli si nzuri. Upande wa Tanzania treni zilichelewa mno, masaa hata siku, lakini hali ilianza kuwa afadhali kuanzia Julai 2016.[9]

Muhimu kwa ajili ya watu ziwani ni huduma ya feri. Kuna meli 2 zinazobeba abiria na mizigo ambazo ni MV Liemba baina ya Kigoma na Mpulungu halafu MV Mwongozo baina ya Kigoma na Bujumbura.
 
Huduma iliyopo hadi sasa ni ngumu na hali za njia za reli si nzuri. Upande wa Tanzania treni zilichelewa mno, masaa hata siku, lakini hali ilianza kuwa afadhali kuanzia Julai 2016.[9]

Muhimu kwa ajili ya watu ziwani ni huduma ya feri. Kuna meli 2 zinazobeba abiria na mizigo ambazo ni MV Liemba baina ya Kigoma na Mpulungu halafu MV Mwongozo baina ya Kigoma na Bujumbura.
 
Eneo hili ni muhimu kimataifa kutokana na bioanwai kubwa: asilimia 10 ya spishi za samaki wote duniani zinapatikana katika maziwa yake.

Maziwa ya Viktoria, Tanganyika na Nyasa hushika robo moja ya maji matamu (yasiyo maji ya chumvi) yaliyopo duniani.
 
Ziwa Nyasa (katika Malawi: Lake Malawi; katika Msumbiji: Niassa) ni kati ya maziwa makubwa ya Afrika ya Mashariki likiwa na nafasi ya tatu baada ya Viktoria Nyanza na Ziwa Tanganyika.

Lina urefu wa km 560 na upana wa km 50-80. Vilindi vyake vinaelekea hadi mita 704 chini ya uwiano wa maji yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…