Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Utapeli upi wa kuvuana picchu au?

4792806544821f7b980a0ca68229ba29.jpg
 
Serikali ya Nigeria inatia aibu kushindwa kuliteketeza genge hilo la kihuni. Genge hilo halina dini wala siasa linatamba kwenye nchi inayosemwa ina nguvu za kijeshi. Pumbafu
Haya mambo ndugu yangu ni magumu. Hawa wanakuwa ni watu mnaoishi nao. Kaka, baba, wana na hata dada. Mchana mnajichanganya nao na muda ukifika hao wanawageuka na kwenda kufanya yao. Ndilo tatizo pia walilokumbana nalo Wamarekani huko Afghanistan. Hujui adui yako ni nani na makamanda wengi wanakiri kuwa vita vya aina hii ndivyo vigumu zaidi kupigana, unless uwe katili uue na raia wasiohusika.

Na wakati mwingine hata kama adui anajulikana, inakuwa vigumu kumtokomeza kutokana na weledi wake wa mazingira aliyomo na umahiri wake wa kujishabihisha nayo. Ndiyo maana mpaka leo Joseph Kony bado yupo na jeshi lake. Kwa nini jeshi la Uganda lisiende tu na kumwangamiza mara moja? Ndiyo maana Dos Antos alihangaika na Savimbi kwa miongo kadhaa. Ndiyo maana kule Colombia waasi wa FARK wamejichimbia msituni huko wanalima coca wanauza na kuendelea kupambana kwa miaka pamoja na madege ya Kimarekani yenye teknolojia ya kila aina kuwasaka mchana na usiku. Afghanistan mataliban wamejichimbia mapangoni huko milimani na Wamarekani hawathubutu kutia mguu huko kwa sababu wanajua kuwa wataangamia. Sana sana wanaishia tu kudondosha mibomu yao ya kilo 500 na kukimbia....

Kwa kifupi, mtu akiamua kujitoa mhanga kupambana na kupigania kile anachokiamini, siyo rahisi kumtoa katika mhimili wake aliojiwekea hata uwe na silaha na jeshi lenye nguvu namna gani. Ndiyo maana migogoro mingi ya aina hii huishia kutatuliwa kwa majadiliano. Na kibaya zaidi, unakuta migogoro hii wakati mwingine inachochewa na hao hao wa upande mwingine kwa sababu zao binafsi, kisiasa na vinginevyo. Ni shida mkuu....
 
Kulainisha maungio/viungo baada ya kulala kwa muda mrefu
Miili yetu hupumzika kufanya kazi tunapokuwa tumelala. Hii ina maana kwamba, kasi ya mapigo ya moyo na mzunguko wa damu hupungua kidogo.
Lakini pia tunapokuwa tumelala, viungo na maungio havifanyi kazi. Haya yote husababisha hali ya misuli na maungio kukakamaa kidogo kwa muda. Tunapoamka asubuhi inashauriwa kujinyoosha ili kuondoa kukakamaa kwa maungio na misuli, pia kurudisha hali ya kawaida ya mzunguko wa damu na kuandaa mwili na shughuli zinazohusisha kujongea/kutembea.
 
Kulainisha misuli na maungio kabla ya kuanza mazoezi
Unapofanya mazoezi, mwili wako hutumia nguvu za ziada. Ili kukabiliana na hilo, mzunguko wa damu unatakiwa kuwa tayari kusafirisha virutubisho vinavyohitajika katika kutengeneza nguvu. Misuli pia inatakiwa kuwa tayari kukabiliana na kazi ya ziada.
Mazoezi ya kunyoosha na kulainisha viungo husaidia kuuandaa mzunguko wa damu na misuli kukabiliana na hitaji kubwa la nguvu, hivyo inashauriwa aina hii ya mazoezi kabla ya kuanza mazoezi ya aina nyingine.
 
Kurudisha misuli, maungio na mzunguko wa damu katika hali ya kawaida baada ya kufanya mazoezi (recovery)
Mara baada ya kumaliza mazoezi, misuli, maungio na mzunguko wa damu huwa katika hali ya kufanya mazoezi. Maana yake mzunguko wa damu huwa mkubwa na misuli huwa imetanuka. Tunapomaliza kufanya mazoezi, misuli na mzunguko wa damu vinatakiwa kurudi katika hali zake za kawaida. Mazoezi ya kunyoosha na kulainisha viungo kama vile ‘stretch ups’ husaidia kurudisha hali hiyo. Kwa maana hiyo, inashauriwa kufanya aina hii ya mazoezi kila baada ya kufanya aina nyingine za mazoezi.
 
Kuzuia magonjwa ya maungio (joint illnesses)
Kutokunyoosha na kulainisha misuli na maungio kwa muda mrefu huweza kusababisha kukakamaa kwa sehemu hizi za mwili. Hii huchangia kutokea kwa magonjwa ya maungio/viungo kama vile Arthritis na mengine.
Maumivu sugu ya mgongo huweza pia kusababishwa na ukosefu wa mazoezi ya kunyoosha na kulainisha viungo. Kujenga tabia ya kufanya aina hii ya mazoezi hutukinga na magonjwa ya maungio (kitaalamu joint illnesses).
 
Ahsante sana aisee kuna group nilikuwa nataka kujitoa kitambo kwani yamejaa MACCM kibao ila kuna watu nikijitoa watalalamika sana maana ni damu damu nimeomba ushauri zaidi ya mara tatu kwa wengine kutaka kujitoa huko lakini wakaniambia usijitoe ila piga kimya maana ukijitoa utalaumiwa sana. Sasa najitoa rasmi kwa mwendo wa kunyatuka nyatuka. Kupiga kimya tu haitoshi nikiona upuuzi wanaopost kuhusu dhalimu DU unanichefua sana.
Ukifuata ushauri huu hautakusaidia. Uki- mute leo, subiri ANGALAU mwezi mmoja yaani mpaka tarehe uliyo-mute ndiyo u-left. Vinginevyo utaonekana tu...

Hata mimi nilikuwa na shida hiyo kwenye group moja hivi la washikaji walioligeuza kuwa kipaza sauti cha Mange. Nilimute nikasepa wakanidaka na kunirudisha. Baadaye ndiyo nikagundua kuwa ni lazima kusubiri kidogo nikamute silently mpaka leo wanajua kuwa bado nipo najadili "upuuzi" wao....

Jiridhishe kwanza kama version mpya uliyonayo haina tatizo hilo vinginevyo jamaa watakurudisha tu na kuendeleza kukulisha utamu wa "dhalimu" [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kupumzisha akili
Mazoezi kama yoga husaidia sana ubongo kupumzika, kitu ambacho ni muhimu kwa afya. Mazoezi ya yoga na mazoezi mengine ya kulainisha na kunyoosha viungo husaidia mzunguko wa damu kuwa mzuri. Hii huongeza kiasi cha damu kinachokwenda kwenye ubongo na viungo vingine, kitu ambacho ni muhimu sana katika kupumzika. Inashauriwa sana kufanya yoga na mazoezi mengine ya kujinyoosha kusaidia mwili kupumzika.
 
Back
Top Bottom