Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Haya mambo ndugu yangu ni magumu. Hawa wanakuwa ni watu mnaoishi nao. Kaka, baba, wana na hata dada. Mchana mnajichanganya nao na muda ukifika hao wanawageuka na kwenda kufanya yao. Ndilo tatizo pia walilokumbana nalo Wamarekani huko Afghanistan. Hujui adui yako ni nani na makamanda wengi wanakiri kuwa vita vya aina hii ndivyo vigumu zaidi kupigana, unless uwe katili uue na raia wasiohusika.

Na wakati mwingine hata kama adui anajulikana, inakuwa vigumu kumtokomeza kutokana na weledi wake wa mazingira aliyomo na umahiri wake wa kujishabihisha nayo. Ndiyo maana mpaka leo Joseph Kony bado yupo na jeshi lake. Kwa nini jeshi la Uganda lisiende tu na kumwangamiza mara moja? Ndiyo maana Dos Antos alihangaika na Savimbi kwa miongo kadhaa. Ndiyo maana kule Colombia waasi wa FARK wamejichimbia msituni huko wanalima coca wanauza na kuendelea kupambana kwa miaka pamoja na madege ya Kimarekani yenye teknolojia ya kila aina kuwasaka mchana na usiku. Afghanistan mataliban wamejichimbia mapangoni huko milimani na Wamarekani hawathubutu kutia mguu huko kwa sababu wanajua kuwa wataangamia. Sana sana wanaishia tu kudondosha mibomu yao ya kilo 500 na kukimbia....

Kwa kifupi, mtu akiamua kujitoa mhanga kupambana na kupigania kile anachokiamini, siyo rahisi kumtoa katika mhimili wake aliojiwekea hata uwe na silaha na jeshi lenye nguvu namna gani. Ndiyo maana migogoro mingi ya aina hii huishia kutatuliwa kwa majadiliano. Na kibaya zaidi, unakuta migogoro hii wakati mwingine inachochewa na hao hao wa upande mwingine kwa sababu zao binafsi, kisiasa na vinginevyo. Ni shida mkuu....
Nilipenda sana Uturuki walivyo deal nao hawa jamaa!
 
Karibu sana Maryland sis.

Mzee Liver atapasuka moyo. Hiyo picha yako tu anavyoilinda imagine eti nikuone laivu. Maweeeeeeeeee !!! Siku hiyo atakodi mamba hapo Nansio na kujitosa ziwani apige makasia kwenda kusikojulikana [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hahahaha uwiii shimba hii kali walahi!
 
Wakenya wamewataka wabunge wao kubeba karatasi zao za kutumia baada ya haja kubwa bungeni iwapo wameghadhabishwa na ukosefu wa karatasi hizo bungeni.
Wabunge katika mjadala siku ya Jumatano walitumia muda wao mwingi kulalamikia ukosefu wa karatasi hizo na maji katika vyoo vyao.
Ni swala lililowaunganisha wabunge wa chama tawala na wale wa upinzani.
Hahahahaha yaani wanasiasa ni shida sana
 
Kiongozi wa walio wachache bungeni John Mbadi alisema kwamba sio maji pekee ambayo hakuna bali hata karatasi hizo.
''Huwezi kuniambia kwamba bunge ambalo wabunge wa taifa wanafanya kazi zao halina karatasi za kwendea haja kubwa na kwamba mara nyengine unaingia chooni na hakuna karatasi hizo''.
Mbadi aliongezea kwamba swala hilo la choo ni tete mno huku mifereji pia ikikosa maji hivyobasi kuwa vigumu kwa wabunge kutekeleza wajibu muhimu wa kuwa wasafi.
Hapo sawa
 
Mtoto wa Kim miaka kumi ijayo

Mtoto: Mama. Najua baba ni mashuhuri kwa sababu ni mmojawapo wa wanamuziki wazuri kabisa.

Kim: Ni kweli. Babako ni mwanamuziki mzuri na ana pesa. Ndicho nilichompendea.

Mtoto: Unajua mama. Sijaelewa umaarufu wako unatokana na nini. Ulifanya nini mpaka ukawa maarufu? Au ulikuwa maarufu baada ya kuolewa na baba?

Kim: Sasa swali gani hilo na wewe? Mitoto mingine hasara tupu. Shwaiiiini [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ouch
Shkamoo Pesa
 
Wakenya wamewataka wabunge wao kubeba karatasi zao za kutumia baada ya haja kubwa bungeni iwapo wameghadhabishwa na ukosefu wa karatasi hizo bungeni.
Wabunge katika mjadala siku ya Jumatano walitumia muda wao mwingi kulalamikia ukosefu wa karatasi hizo na maji katika vyoo vyao.
Ni swala lililowaunganisha wabunge wa chama tawala na wale wa upinzani.
Halafu tukiitwa shithole na akina Trump tunakasirika [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
kp23022018.jpg
BAK BAK
 
Back
Top Bottom