Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mnafanana kila kitu. Hii ni mbinu nyingine wanaitumia kuisimamia akili yako. Mara ya kwanza kukutana atakwambia kuwa anapenda kila kitu ambacho unapenda. Utajua ukweli wa haya maneno kwa jinsi anavyokujibu. Mfano ukimwambia kitu atakujibu, "Pia mimi."
 
Anakupa heko kupita kiasi. Kuna wakati mwingine kutoa heko inafikia mahali kunapita kiasi. Mwanamke aina hii utamwona anakusifia kwa kila kitu. Ukifanya jambo flani anakusifia, ukifanya lile anakusifia, hata kupiga mswaki anakwambia, "Leo bebi umeng'ara meno" Hapo jua fika kuwa anauangalia mfuko wako zaidi ya pendo lako
 
Kisa cha mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu nchini Tanzania kuuwawa kwa risasi wakati polisi ya nchi hiyo ilipokuwa ikitawanya kile walichokiita mkutano usio halali wa wafuasi wa upinzani kimeibua maswali na hisia kali miongoni mwa umma juu ya kiwango cha nguvu ambacho polisi hutumia wanapokabiliano na waandamanaji.
Maelezo ya kifo cha msichana huyo yamedai hakulengwa moja kwa moja kwa sababu hakuwa sehemu ya waandamanaji wala kitisho kwa usalama.
 
Lakini polisi wameshutumiwa kwa kutumia risasi za moto zilizosababusha kifo chake. Polisi wenyewe wanasema uchunguzi bado unaendelea kubaini aliyehusika na kifo hicho.
 
Lakini Tanzania haiko peke yake. Aghalabu idara za polisi katika nchi nyingi za Afrika zimejipata lawamani katika mikasa mingi ya aina hiyo kwa kutumia nguvu kupita kiasi wakati wa kudhibiti fujo na ghasia ikiwemo matumizi ya silaha za moto ambazo taathira zake huwa kifo au majeraha ya kudumu kwa aliyelengwa.
 
Kwa muda mrefu kumekuwa na mjadala juu ya iwapo maafisa wa polisi barani Afrika hupatiwa mafunzo madhubuti na vifaa vya kisasa kukabiliana na uhalifu, fujo na ghasia bila kuhatarisha usalama wao binafsi na wale wanao wadhibiti.
 
Mjadala wa aina hii umehanikiza zaidi juu ya namna polisi inavyodhibiti mikusanyiko ya kiraia kama maandamano ambayo inatazamwa kuwa haki za msingi za raia kuliko jinsi polisi inavyokabiliana na matukio kama ujambazi na uporaji.
 
Sehemu kubwa ya lawama kwa polisi karibu kwenye matukio yote hususan ya maandamano ya raia, wanakosolewa kwa kutumia nguvu kubwa dhidi ya watu wasio na silaha na tena katika mazingira ambayo mbinu nyepesi zingeweza kusaidia kurudisha utulivu.
 
Hali ikoje barani Afrika?
Ingawa suala la polisi kulenga raia kwa silaha za moto ni la kilimwengu ukipigia mfano wa matukio kama hayo nchini Marekani dhidi ya raia weusi, hali ni dhaifu zaidi kwenye nchi maskini na zaidi Afrika ambapo ni nadra makosa kama hayo kuripotiwa au wakosaji kushughulikiwa kisheria.
 
Kulingana na ripoti ya karibuni kabisa ya mwaka 2016/2017 ya shirika la Amnesty International, Kenya ndiyo nchi inayoongoza kusini mwa jangwa la Sahara kwa visa vya polisi kuua au kujeruhi raia kwa kutumia risasi za moto.
 
Ripoti hiyo ilizitaja pia nchi nyingine tatu wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki za Tanzania, Burundi na Sudani Kusini kuwa miongoni mwa mataifa vinara ambayo polisi wanatumia nguvu kupita kiasi na kuwakandamiza zaidi wafuasi wa upinzani.
 
Back
Top Bottom