JE huyu mwanamke ana athari gani kwa maisha yako?
Ok. Wanaume wengine wangesema hawana tatizo na kuwa na mwanamke aina hii. Kama pesa niko nazo ya nini nilalamike? Mwache azitumie mpaka achoke yeye. Well, hapa Nesi Mapenzi tuna mtizamo tofauti. Mwanamke anayejitokeza kama gold digger huwa anatumia saikolojia kukuteka nyara kiakili na mawazo. Atatumia mbinu fioa za kukuzuzua kiasi cha kuwa kila kitu akitaka utampa bila wewe kufikiria. Na ukikataa ama kama umeishiwa na hela siku moja au nyingine atakunyima kitu ambacho umezoea kupata kutoka kwake. Mfano wa gold digger leo ukimwambia sina pesa za kukununulia simu ya iPhone X, siku ya pili hatopokea simu yako ama mbaya zaidi atakuwekea mgomo baridi usikaribie tunda lake. Upo!? Hebu tuziangalie baadhi ya tabia za huyu mwanamke gold digger.