Sikuwa na taarifa yoyote ya kuhudhuria mkutano huo, na nilipangiwa kazi na mkuu wangu ambaye ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, nitembelee na kukagua miradi mbalimbali ya Serikali mkoani Kigoma,” alisema kwa simu jana.
Ulega alisema hakuwa na taarifa yoyote kama Rais aliuliza uwapo wa viongozi wa wizara hiyo wakati wa mkutano huo, “Nilikuwa ndani ya ndege tangu saa nane mchana nilipotoka Kigoma na hadi muda huu (saa 10 alasiri) unanipigia simu ndiyo kwanza nashuka kwenye ndege.”

Wakati viongozi hao wa wizara ya mifugo wakitoa maelezo hayo, Dk Tizeba na naibu wake, Mary Mwanjelwa hawakutaka kuzungumza lolote kuhusu kikao hicho wakisema walikuwa kwenye kikao.
Hii si mara ya kwanza kwa mawaziri hawa kuingia matatani. Katika mkutano wa Bunge wa Februari, Mpina na Dk Tzeba waliwekwa ‘kitimoto’ baada ya wabunge baadhi yao kuibua hoja mbalimbali dhidi yao wakati wakichangia taarifa za utekelezaji wa shughuli za kamati mbili za kilimo, mifugo, maji na Ardhi, Maliasili na Utalii.

Mbunge wa Busega (CCM), Dk Raphael Chegeni alimshukia Mpina akisema anakuwa na kiburi na kumtaka aache kwa kuwa anawaumiza wafugaji.
Hata hivyo, Mpina alijibu ‘mashambulizi’ yaliyoelekezwa kwake akisema ataendelea kufanya kazi kwa weledi bila woga wa kumshughulikia mtu yeyote anayekwenda kinyume cha sheria.
Dk Tizeba alishambuliwa na wabunge wanaotoka katika ukanda wa kilimo cha mahindi waliotaka kujua mkakati wa Serikali wa kuongeza bei ya mahindi.
Hata hivyo, kiu ya wabunge hao haikukatwa baada ya Dk Tizeba kuweka msimamo kuwa mazao hayo yanasimamiwa kwa mujibu wa sheria.
Dk Tzeba pia aliwahi kukutana na joto la Dk Magufuli Januari mwaka huu wakati Rais akimwapisha Doto Biteko kuwa naibu waziri wa madini.
Rais Magufuli alisema haiwezekani baadhi ya mikoa, ikiwamo inayotegemewa kwa uzalishaji wa chakula kwa wingi, kushindwa kupata mbolea, huku yeye (Dk Tizeba) akiwa hajachukua hatua.

JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.