Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mkutano huo uliwakutanisha wafanyabiashara na watendaji waandamizi wa Serikali, lakini mawaziri wawili, Dk Charles Tizeba (Waziri wa Kilimo) na Luhaga Mpina (Mifugo na Uvuvi) hawakuhudhuria huku Rais akiwa hana taarifa zao na hawakutuma wawakilishi kwenye mkutano huo.
 
Kutokuwapo kwa mawaziri hao kulibainika baada ya Rais Magufuli kumtaka Mpina ajibu masuala mbalimbali yaliyoibuliwa na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Asas Dairies ya Iringa, Fuad Abri kuhusu bidhaa za maziwa. Pia alitaka ataje idadi ya viwanda vya maziwa vilivyopo hapa nchini.
 
Hata hivyo, si waziri huyo, wala mwakilishi yeyote kutoka wizarani kwake aliyekuwapo kwenye mkutano huo wa kumi na moja wa baraza hilo na ndipo Rais Magufuli alipomtaka waziri wa kilimo kujibu swali hilo kwa sababu alikuwa akisimamia wizara hiyo kabla ya kuitenganisha. Hata hivyo, naye hakuwapo na hapakuwa na mwakilishi yeyote.
 
Mawaziri wote wanaoguswa na sekta za uwekezaji na hasa kwenye uchumi huu wa viwanda, kilimo ni facilitator (mwezeshaji) wa viwanda, mifugo nayo pia ni viwanda. Walikuwa wanapaswa kuwepo hapa kwa sababu walishapewa taarifa wote,” alisema Majaliwa.
 
Mawaziri wote wanaoguswa na sekta za uwekezaji na hasa kwenye uchumi huu wa viwanda, kilimo ni facilitator (mwezeshaji) wa viwanda, mifugo nayo pia ni viwanda. Walikuwa wanapaswa kuwepo hapa kwa sababu walishapewa taarifa wote,” alisema Majaliwa.
 
Rais Magufuli alisema inasikitisha kuona baadhi ya watu aliowateua hawajaelewa anataka nini. Alisema inashangaza kuona wafanyabiashara kutoka sehemu mbalimbali nchini wamekutana na Serikali kuzungumzia masuala ya kilimo na mifugo, lakini mawaziri wa sekta hizo hawapo.
 
Tunaongelea mambo ya kilimo na mifugo, lakini waziri au katibu mkuu hayupo hapa, itabidi waziri mkuu achukue hizi kero zenu akazifanyie kazi,” alisema Rais Magufuli na kumtaka Waziri Mkuu Majaliwa kuunda timu itakayowahusisha mawaziri wanaohusika ili wakayafanyie kazi malalamiko yaliyoibuliwa na wafanyabiashara katika mkutano huo.
 
Back
Top Bottom