andjul
JF-Expert Member
- Dec 14, 2013
- 19,383
- 121,663
Ile oven pembeni kulikuwa na samaki na kiganja cha mbaba "mwenye nguvu" ni kiwanda?Hata oven yako ni kiwanda ujue
Hata tukiwa na umeme wa maana bado hatutafanikiwa ikiwa ushabiki wa kisiasa upo kila kona mpaka imefikia hatua ya kubaguana sio maofisin majumban wala mikutanon,misiban pote shida tupu
Sijui watanzania tunapenda sana siasa?
Nilikuwa kijijini kwa bibi yangu kwa wiki kadhaa mwezi uliopita,watu hawajishughulishi kama zamani,ni wavivu kupindukia.Muda mwingi ni hadithi za vyama vya siasa na mipira ya ulaya...
Inawezekana huyu kiongozi hatuja muelewa,labda kwa vile tulizoea maisha ya kuiomba serikali itusaidie hata kufukia madimbwi yanayo zunguka makazi yetu na vyandarua vya bure wakati tunasubiria kufukiwa madimbwi hayo.
Inawezekana kiongozi huyu hajatuelewa kuwa tunapenda sana siasa(porojo) kuliko kitu kingine chochote,au ametuelewa ila anataka kututoa huko kwenye kupenda siasa(porojo) na kutufanya tupende kufanya kazi za kutuongezea kipato.
Naamini ipo siku atakuja kutuelewa...
Naamini ipo siku tutakuja kumuelewa...
Vyovyote itakavyo kuwa,maumivu yatakuwa kwa "Mswahili".