Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

BgY_Lx9gjYd.jpg
 
Serikali imesema wanafunzi wa vyuo vikuu wanaongoza kutukana na kutumia lugha zisizo na maadili kwenye mitandao ya kijamii.

Angalizo hilo limetolewa na naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha jana Jumamosi Machi 24, 2018 katika hafla fupi ya uzinduzi wa Unilife Compus iliyopo Mkoa wa Kilimanjaro uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Mwenge na kuvikutanisha vyuo vikuu vyote vya mkoa huo.
 
Amesema yapo mambo matatu ambayo yanachangia wanafunzi kutofanya vizuri, yakiwamo matumizi mabaya ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), anasa na starehe zilizopitiliza na kujiingiza kwenye siasa ambazo zinawanyima fursa ya kusoma vizuri.
 
Serikali imebaini mambo yanayochangia kufifisha na kudidimiza jitihada za elimu tunayoitoa kuonekana bure. Kuna vitu ambavyo siyo vizuri vinaendelea katika vyuo vyetu, ndizo changamoto tunatakiwa kukabiliana nazo. Chuoni unaweza kutengeneza au kuharibu maisha yako,” amesema.
 
Naye mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema wanafunzi wengi hawataki kujifunza kwa kutumia muda vizuri kwa kusoma vitabu.

"Tunabaki kuwa waigaji wa dhana za wenzetu wa magharibi, hatutaki kujifunza vitu vipya bali vilevile vya wenzetu vinatumika hadi leo. Wasomi wa Tanzania tunajishusha kwa sababu ya kushindwa kuleta mawazo mapya kwenye sekta ya elimu na afya," amesema Mghwira.
 
Baada ya utafiti kubaini mwamko mdogo kwa wanaume kupima na

kutumia dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi (ARVs), Tume ya

Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) sasa kuanzisha kampeni maalumu.
 
Akizungumza leo Jumapili Machi 25, 2018 na Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Kupambana na Dawa za Kulevya, mkurugenzi mkuu Tacaids, Dk Leonard Maboko amesema kampeni hiyo itakuwa miongoni mwa shughuli zitakazofanywa katika mkakati wa nne wa kupambana na Ukimwi nchini.
 
Katika utafiti wa mwaka 2016/17, tuliangalia vitu vipya ambavyo ni

maambukizi mapya na kiwango cha kufubaza VVU. Tuligundua ingawa wanawake wanaongoza katika maambukizi mapya, lakini ni wepesi kupima na kutumia dawa kikamilifu ndiyo maana kwenye kiwango cha kufubaza wanaongoza,”amesema.
 
Amesema katika utafiti huo uliozinduliwa Desemba mwaka jana, kiwango

cha watu kufubaza VVU kwa wenye miaka kati ya 15 na 64 ni asilimia 52 lakini kati ya hao, 57.5 ni wanawake na wanaume ni 41.2.
 
Naye waziri wa nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera), Jenista Mhagama amesema mwaka 2015 wafadhili wa tume hiyo walianza kupunguza fedha

za mapambano dhidi ya VVU.
 
Tetemeko la ardhi lililodumu kwa takribani dakika moja usiku wa kuamkia leo Machi 25, 2018 limetokea Mkoa wa Mwanza, Kagera na Geita, kuzua taharuki kwa wakazi wa mikoa hiyo, huku baadhi wakijaribu kukimbia nyumba zao kwa nia ya kujiokoa.
 
Hata hivyo hakuna madhara ya vifo au uharibifu ulioripotiwa hadi jana.

Jiolojia Mwanandamizi kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Gabriel Mbogomi amesema tetemeko hilo lina ukubwa wa richa 4.6 na lilikuwa likitokea Kaskazini Magharibi ya Mji wa Kahama kuelekea kusikojulikana.
 
Kwa mujibu wa GST, Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazotokewa na tetemeko la ardhi kutokana na kuwa sehemu ya mkondo wa Bonde la Ufa.
 
Chama cha Waajiri Afrika Mashariki(EAEO) kimesema nusu ya wahitimu wa vyuo vikuu katika nchi za Afrika ya Mashariki wanakosa sifa na ujuzi wa kuajiriwa.

Wakizungumza jana Jumamosi Machi 24, 2018 katika mkutano wa nne wa mwaka wa EAE0, Katibu Mkuu wa EAEO,Dk Aggrey Mlimuka na mwenyekiti wake Rosemary Ssenabulya, wamesema ni muhimu tatizo la kukosa sifa za kuajiriwa kwa wahitimu hao kufanyiwa kazi na wadau wote.
 
Dk Mlimuka amesema tafiti ambazo zimefanywa zinaonesha kuwa vyuo vikuu na vyuo vya kati katika nchi zote za Afrika Mashariki vinatoa elimu ambayo inawafanya vijana washindwe kuajiriwa.

Amesema ili kukabiliana na tatizo hilo, lazima vyuo viweze kuandaa vyema wahitimu kwa kuwepo na mahusiano baina ya mitalaa ya masomo na mahitaji katika soko la ajira.
 
Nilimsikia Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa akielezea jambo hili napenda kueleza tatizo hili lipo katika nchi zote lazima sasa mafunzo ya vyuo yajibu changamoto sehemu za kazi na kuwapa ujuzi wahitimu,” amesema.
 
Back
Top Bottom