Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Matunda yaliyo kaushwa
Matunda yaliyo kaushwa ni muhimu sana kwa maana hua na vitamini, fiber na madini zaidi kulinnganisha na matunda ambayo hayajakaushwa na hivyo kuongeza utengenezaji wa misuli kwa kuongea calorie nyingi mwilini. Hivyo basi inashauriwa kula japo mara mbili na zaidi ilikuhakikisha ukuaji wa mwili
 
Viazi
Viazi ni aina ya vya vyakula ambavyo hutajika sana mwilini kwa mtu ambaye anayetamani kuongeza mwili, Mbali na sifa zake za kuwa na uwezo wa kusaidia misuli ya mwili kwenye uhifadhi glycogen, viazi hua na fiber na madini mengi. Hivyo basi ningependa kushauri watu wengi kutumia viazi hasa wenye kutaka kujenga miili kwa vyuma.
 
Kunenepa ni kitu kizuri, lakini ni vizuri sana kunenepa kwa kufuata njia bora za afya ili uendelee kuufanya mwili kunawiri kuliko kufikia malengo kwa kuharibu mwili moja kwa moja. Unaweza kujaribu njia chache kati ya hizi ili uangalia ipi inafanya kazi vizuri kwako.
 
Kula mara nyingi zaidi
Uzito wa miili yetu hutegemea sana kiasi cha chakula bora tunachokula. Wengi tumezoea kula mara tatu kwa siku. Tatizo huja pale ambapo unakuwa huli chakula kingi sana kwa kila mlo, maana mwili unakosa kupata virutubisho vya ziada vya kuhifadhi mwilini.
 
Ni muhimu pia kufahamu kuwa vyakula vingi vinavyonenepesha hushibisha haraka sababu ya uwepo wa mchanganyiko wa virutubisho vingi mfano nyuzi nyuzi (fiber), ambazo hukufanya ushibe haraka na kwa muda mrefu zaidi. Hivyo, kula kidogo kidogo mara nyingi kunaweza kusaidia kuongeza uzito.
 
Kula nafaka zisizokobolewa
Mwili unaohitaji virutubisho unatakiwa kula vyakula vilivyojaa virutubisho. Vyakula vilivyokobolewa mara nyingi huwa na virutubisho vichache, na huwa havileti afya sawa na vile visivyokobolewa. Hivyo, kula vyakula visivyokobolewa. Tumia bidhaa zilizotengenezwa na nafaka zisizokobolewa – mkate wa ngano isiyokobolewa, ugali wa dona, maharage n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…