Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Everton wana mzozo wa mkataba na meneja wa zamani wa timu hiyo Ronald Koeman, ambaye kwa sasa ni meneja wa timu ya Uholanzi Netherlands, baada ya kubainika kuwa kilabu hicho kinalipa 90% ya malipo aliyolipwa Muholanzi huyo. (Liverpool Echo)
 
Watford huenda wakamuuza kwa kiwango cha Euro milioni 40 mchezaji wa kiungo cha kati Abdoulaye Doucoure, mwenye umri wa miaka 25, katika msimu huu wa majira ya joto, huku Liverpool, Tottenham na Arsenal wote wanammezea mate mFaransa huyo. (Mirror)
 
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Stoke Ibrahim Afellay, mwenye umri wa miaka 31, ameambiwa awe mbali na klabu hiyo na Paul Lambert, ambaye hapendezwi na tabia ya Mholanzi huyo na kiwango chake katika mazoezi. (Telegraph)
 
Winga wa Real Madrid Gareth Bale, mwenye umri wa miaka 28, ameshawishiwa na meneja wa Manchester United Jose Mourinho kujiunga na klabu hicho ya Ligi ya Premia mwisho wa msimu. (Marca)
 
Wakati huo huo, Bale ameambiwa na kocha wa Wales Ryan Giggs aendeshe kiti maalum ili kujiepusha na majeraha. (Times)
 
Striker Zlatan Ibrahimovic, mwenye umri wa miaka 36, aliondoka Manchester United baada ya kushindwa kuendelea katika ligi ya klabu bingwa Ulaya, kulingana na daktari aliyemfanyia upasuaji ya goti la mchezaji huyo wa Sweden. Amejiunga na LA Galaxy. (South China Morning Post)
 
Manchester United wanaangalia uwezekano wa kusaini mkataba na mchezaji wa kiungo cha kati wa Tottenham Chukwunonso Madueke, mwenye umri wa miaka 16, baada ya kukataa kusaini mkataba mpya na kilabu hicho cha kaskazini mwa London. (Mail)
 
Meneja wa Italia Carlo Ancelotti amekataa kuchukua kazi ya kuiongoza timu ya taifa hilo kwani anasubiri kurejea katika Ligi ya Premia ya Ulaya, huku chaguo lake likiwa ni klabu za Chelsea na Arsenal (ItaSportPress - kwa Kitaliano)
 
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Juventus Claudio Marchisio, mwenye umri wa miaka 32, anaweza kuondoka katika kilabu hicho kujiunga na MLS ya New York City. Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia katika Turin unamalizika msimu huu wa majira ya baridi. (Tutto Mercato Web - in Italian)
 
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Juventus Claudio Marchisio, mwenye umri wa miaka 32, anaweza kuondoka katika kilabu hicho kujiunga na MLS ya New York City. Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia katika Turin unamalizika msimu huu wa majira ya baridi. (Tutto Mercato Web - in Italian)
 
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Bournemouth Lewis Cook, mwenye umri wa miaka 21, alimfanya babu yake tajiri wa Euro 17,000 alipochezea kwa mara ya kwanza England dhidi ya Italia siku ya Jumanne. Trevor Burlingham aliweka dau la Euro 500 mnamo mwaka 2014 juu ya ushindi wake kabla hajatimiza umri wa miaka 26. (Telegraph)
 
Mkurugenzi wa soka wa timu ya Aston Villa Steve Round anasema nahodha John Terry ameashiria kuwa ataendelea kuwa na kilabu hicho. Mlizi huyo wa zamani wa England, mwenye umri wa miaka 37, amekuwa akitarajiwa kustaafu na kurejea katika kilabu cha Chelsea kama kocha. (Birmingham Mail)
 
Mwanasiasa wa upinzani Kenya aliyeidhinisha kiapo cha kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuwa 'Rais wa Wananchi' Januari Miguna Miguna ametimuliwa tena kutoka nchini humo.
Mwanasiasa huyo ametimuliwa huku mzozo kuhusu uraia wake ukiendelea.
Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu, Tume ya Taifa ya Haki za Kibinadamu Kenya (KNCHR) na shirika la kimataifa la Human Rights Watch wameishutumu hatua ya serikali ya kuendelea kumzuia Bw Miguna kurejea Kenya.
Bw Miguna asubuhi aliandika kwenye Facebook kwamba aliamka na kujipata yuko Dubai na kwamba anahitaji matibabu.
Alisema anafahamu kwamba kuna mpango wa kumpeleka London lakini alitaka kupanda ndege ya kurejea Nairobi pekee.
Mwanasiasa huyo alisema alisindikizwa na afisa wa idara ya ujasusi na kwamba amemuona daktari uwanja wa ndege.
Bw Miguna alisisitiza kwamba hatasafiri kwenda popote ila kurejea Nairobi.
 
Jaji wa Mahakama Kuu George Odunga Jumatano alisema waziri wa usalama nchini humo, mkuu wa polisi na mkuu wa idara ya uhamiaji watakuwa wamekaidi maagizo ya mahakama iwapo wangekataa kumwachilia huru.
Alikuwa ametoa ilani kwa watatu hao kufika mahakamani baadaye Jumatano lakini baada yao kukosa kufika akawapata na hatia ya kukaidi agizo la mahakama.
Aliahidi kutoa adhabu dhidi yao leo asubuhi lakini kikao kilipoandaliwa akatoa muda kwa mawakili wa serikali kujaribu kuona iwapo maafisa hao watatii agizo la mahakama kabla ya kuwaadhibu.
Maafisa wa Kenya mnamo 6 Febuari walikuwa wamemfukuza kutoka nchini humo kutokana na mchango wake wakati wa kuapishwa kwa Bw Odinga.
Walisema mwanasiasa huyo hana uraia wa Kenya lakini ana uraia wa Canada.
Idara ya uhamiaji ya Kenya imekariri kuwa Miguna alipoteza uraia wa Kenya mwaka 1998 alipopewa uraia wa Canada wakati ilipokuwa ni kinyume cha sheria kuwa na uraia wa nchi mbili nchini Kenya.
 
Back
Top Bottom