Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ni aje Mkuu andjul?
Safi BAK [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120] hongera kwa kumaliza kifungo salama.
Kuna comment ulituachia,bado ina hitaji ufafanuzi wa kina...yaani kukazia kilichomo...namaanisha msisitizo wa haja[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Niifukue? Kwa heshima yako mkuu[emoji120] [emoji120] Nina shida na pale pa "kutetemeka"
 
Watu wanaochora kwenye Mwamba:

Hawa ni wale ambao hasira ikiwajia inakaa ndani yao kwa muda mrefu. Kama vile unapochora mwamba inachukua muda sana kufutika. Mpaka upepo, maji na hali ya hewa kubadilisha mchoro uliopo kwenye mwanga basi hata aina hii ya watu hasira yao inachukua muda kuondoka na wanateseka nayo bila kujijua.
 
Watu wanaochora kwenye udongo/ardhi.

Aina hii ya watu wenye hasira nao wanapata hasira, na hasira ikiwaingia haikai muda mrefu sana. Kama vile uchorapo kwenye udongo, mchoro utafutika lakini hautakaa sana.
 
Watu wanaochora kwenye maji;

Hawa ni wale ambao hasira ikiwaingia haikai, kwani wanaitambua hasira pale inapokuja lakini hawajishikilii nayo. Hasira inakuja na kupita papo hapo. Kama vile ilivyo vigumu kuchora kwenye maji basi ni vigumu pia kuwa na hasira kwa aina hii ya watu.
 
Tunachopaswa sio kutokuwa na hasira kwani ni vigumu kutokuwa na hasira, bali tunapaswa kuitambua hasira inapokujia, na kuhakikisha hasira hiyo haikuongozi bali wewe ndiye kiongozi wake. Usikubali hasira ikutawale, usikubali kufanya maamuzi kwa hasira.
 
IMG_20180329_213352_031.jpg
 
Back
Top Bottom