Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

UTAYALISHAJI WA MBEGU
Mbegu za maboga zinatoka ndani ya maboga, kuna mbegu zilizoboreshwa (za kisasa) na za asili, andaa mbegu mapema wiki moja au mbili kabla ya kupanda.
 
MATANDAZO (MULCHES )
Kwasababu ni zao linalotambaa basi lazima tuangalie namna ya kutandaza, weka nyasi na mabaki ya mimea mingne kufunika ardhi.
 
Baada ya miche kutambaaa kwa kiasi unaweza kuweka matandazo (mulches) ambayo yaweza kuwa nyasi kavu kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu vile viile kupunguza uotaji wa magugu shambani kwako. Vile vile matandazo yakioza yanaongeza rutuba kwenye udongo na hulinda udongo dhidi ya mmomonyoko wa udongo.
 
MBOLEA
Katika matumizi ya mbolea yanatofautiana kutokana na mbegu, Lakini tumia mbolea za asili (samadi au mboji) ili kuongeza rutuba kwenye udongo, ukihitaji kutumia mbolea za viwandani weka kiasi sana, labda eneo hilo kama hakuna rutuba, mbolea ya NPK inaweza tumia.
 
UPALILIAJI & UNYEVU
Palilia shamba nyasi zinapoanza kuota, pia safisha shamba ili kuondoa wadudu. Shamba la maboga linatakiwa liwe na unyevunyevu kila mara ili maboga yaweze kustawi vizuri yasidumae.
 
UVUNAJI
Maboga hukomaa baada ya siku 95 mpaka 120, ili kujua kuwa boga lako limekomaa unaangalia kikonyo, kikonyo cha boga kinapoteza maji na kinaanza kuwa kikavu.
 
Zao la muhogo ni muhimu sana kwa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Wakulima wengi huchanganya zao la muhogo na mazao mengine kama vile kunde, mbaazi, njugumawe, n.k. Umuhimu wa zao hili ni kutupatia chakula na wakati mwingine kwa biashara. Kwa kanda ya kusini muhogo ni chakula kikuu ambacho kinachukua asilimia 75 ya chakula kwa maeneo yote ya mikoa ya pwani
 
Muhogo hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye maeneo ya mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Vile vile muhogo hustawi vizuri kwenye aeneo yanayopata mvua ya wastani wa mm 750 - mm1200 kwa mwaka. Muhogo hustawi vizuri kwenye ardhi ya kichanga. Vili vile zao la muhogo ni maarufu sana kwa uvumilivu wa hali ya ukame.
 
MBINU BORA ZA KILIMO CHA MUHOGO

· UANDAAJI WA SHAMBA

Shamba liandaliwe kabla ya msimu wa kuanza. Uandaaji wa shamba bora hufuata hatua zifuatazo:

- Kufyeka shamba

- Kung’a na kuchoma visiki

- Kulima na kutengeneza matuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…