Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Lakini, soka ni biashara, hivyo kwenye kila kikosi kinatazamwa nini kimekusanywa au kimetoka ama kwa kuuza wachezaji au kusajili. Utafiti uliofanywa na kampuni ya CIES Football Observatory kuhusiana na thamani ya vikosi, umeweka hadharani thamani ya kikosi cha Man United kwa sasa kulingana na thamani za wachezaji wao zilivyo huko sokoni kwa sasa.
 
Wachezaji waliopanda thamani

Wachezaji ambao thamani zao zimepanda ni Nemanja Matic, aliyesajiliwa kwa Pauni 40 milioni, lakini ukitaka saini yake kwa sasa ni Pauni 55.9 milioni. Scott McTominay ametokea kwenye akademia, lakini ukumhitaji kumsajili lazima utoa Pauni 12 milioni, huku Sanchez, aliyenaswa kwa thamani ya Pauni 36 milioni, ukimhitaji kwa sasa basi itakulazimu kulipa Pauni 85.1 milioni.
 
Straika Romelu Lukaku alinaswa kwa Pauni 75 milioni, lakini ukitaka kumnunua kwa wakati huu, utapaswa kulipa Pauni 142.2 milioni, wakati Anthony Martial alisajiliwa kwa Pauni 36 milioni na ukimtaka kwa sasa utalazimika kulipa Pauni 72.8 milioni kutokana na thamani yake sokoni. Marcus Rashford ametokea kwenye akademia, lakini soko la sasa linamtambua kuwa na thamani ya Pauni 96.5 milioni, huku David De Gea, aliyenaswa kwa Pauni 18.9 milioni, ukihitaji huduma yake kwa sasa utalazimika kulipa Pauni 41.1 milioni, hivyo ndiyo thamani yake kwenye soko kwa wakati huu.
 
Kipa Sergio Romero alitua Man United bure kabisa, lakini kwa sasa thamani yake ni Pauni 4.7 milioni, sawa na ilivyotokea kwa Joel Pereira aliyejiunga na timu hiyo bure na thamani yake kwa sasa ikipanda na kuwa Pauni 5.1 milioni. Beki wa kati,
 
Victor Lindelof alisajiliwa kwa Pauni 31 milioni, lakini soko kwa sasa linamtambua kuwa na thamani ya Pauni 44.2 milioni na Eric Bailly alisajiliwa kwa Pauni 30 milioni na thamani yake kwa sasa ni Pauni 42.9 milioni. Mabeki wengine,
 
Lakini, soka ni biashara, hivyo kwenye kila kikosi kinatazamwa nini kimekusanywa au kimetoka ama kwa kuuza wachezaji au kusajili. Utafiti uliofanywa na kampuni ya CIES Football Observatory kuhusiana na thamani ya vikosi, umeweka hadharani thamani ya kikosi cha Man United kwa sasa kulingana na thamani za wachezaji wao zilivyo huko sokoni kwa sasa.
 
Phil Jones thamani yake imepanda na kufikia Pauni 17.6 milioni, wakati alisajiliwa kwa Pauni 16.5 milioni, huko Marcos Rojo aliyenaswa kwa Pauni 16 milioni sokoni kwa sasa thamani yake ni Pauni 18.8 milioni huku Chris Smalling thamani yake imepanda hadi Pauni 20.3 milioni kutoka Pauni 10 milioni zilizotumika kupata huduma yake. Kiungo, Pogba alinaswa kwa Pauni 89 milioni na thamani yake kwa sasa sokoni ni Pauni 127.2 milioni. Hata kinda, Cameron Borthwick-Jackson aliyeibukia kwenye akademia, thamani yake kwa sasa ni Pauni 2.3 milioni. Jesse Lingard thamani yake kwa sasa ni Pauni 48.9 milioni, wakati akiwa ametokea kwenye akademia.
 
Wachezaji walioshuka thamani

Kiraka wa Kidachi, Daley Blind ni mmoja wa wachezaji ambao thamani yao sokoni imeshuka kwa kiasi kikubwa ambapo staa huyo alisajiliwa kwa Pauni 13.8 milioni, lakini sokoni kwa sasa thamani yake ni Pauni 11.7 milioni. Luke Shaw, wakati anatua Man United alilipiwa Pauni 27 milioni, lakini kwenye soko la usajili kwa sasa thamani yake ni Pauni 10.3 milioni, huku Antonio Valencia thamani yake imeshuka hadi Pauni 8.7 milioni wakati ilimsajili kwa Pauni 16 milioni.
 
Back
Top Bottom