Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unalo kusudi. Unayo zawadi uliyopewa na Mungu, lakini bado hujaigundua kwa sababu ya kukosa uwezo wa kujitambua. Unaweza ukakutana na changamoto nyingi ,magumu, kupoteza , lakini kumbuka kuna kuamka tena, hutaweza kulala moja kwa moja. labda kama utakuwa umeondoka Duniani.
 
Kila mtu yupo tofauti, kuna mnene na kuna mwembamba, Kuna weupe na weusi. Ukiweza kutambua jinsi gani kila mtu ni wa tofauti utaanza kujikubali.Kuna mtu ambaye ni mwepesi kujifunza jambo jipya, lakini kuna mtu mwingine mpaka asukumwe kujifunza kwa faida yake mwenyewe.
 
Hivi hujawahi kujiuliza kwa nini watu wengine wanafanya vizuri na wakati hawana Elimu. Lakini wengi wenye Elimu nzuri hawafanyi vizuri katika mambo mengi? Hujawahi kujiuliza kwa nini unarudia jambo hilo hilo kila mara wakati halina faida kwako? mimi nimewahi kujiuliza zaidi ya miaka 20.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…