Sijui tu tatizo ni nini aisee, na kabla ya kufanikiwa mtu anajiapiza kila siku, "Nikifanikiwa wazazi/mzazi wangu atafurahia, ntamfanya kuwa mtu kati ya watu.
Lakini akishafanikiwa, utashangaa na roho yako, yeye kumtumia bi mkubwa pesa ya sukari na sabuni ndo kamaliza,, mzazi nyumba yavuja maji, ndani bado anatumia viti vya kukunja, mafua na vikohozi havimuishi/haviwaishi kwa vumbi lililojaa ndani....
Mtoto huko aliko anajulikana karibu sehemu zote za starehe na amekuwa na roho nzuri sana kwa makahaba wa mjini wasiojua katoka wapi na kafikaje pale, wao busy tu kumkandakanda....[emoji48][emoji48]
Halafu limtu kila siku likienda mjini ni kutoa ahadi zisizo na mashiko, zisizo tekelezeka...
Wafikiri Amani itadumu kwao???? Hata kidogo..
Wanaume wengi hili limekuwa tatizo kubwa kwao...kwa watoto wa kike Alhamdullilah kidogo tunachopata tunagawana na mzazi/wazazi wetu...Hata hizo wanazodanga kwenu, nusu yaenda nyumbani, nusu yasukuma maisha yao.
Mwenyezi Mungu awaponye.