Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Dini ni imani ndiyo, lakini kuna muda huwa nikijaribu kufikiri sana kuhusu ujio/uwepo wa dini (Ukristo/Uislamu) nakuwa napata shida kujua ukweli uliojificha ndani ya imani hizi.

Kwa upande wa ukristo, dini/neno la Mungu lipo ili kuelezea uwepo wa Mungu, uumbaji wa mbingu na nchi na vitu vilivyomo, chanzo cha uasi (dhambi), wokovu. Kukawa na wachungaji, mapadree n.k ili kutukumbusha kile kilichoandikwa kwenye Biblia. Hivyo tumeagizwa tulitii na kulifuata neno la Mungu.

Vile vile kwa suala la ubatizo (Maji mengi/machache)
Maandiko yanasema binadamu tunazaliwa na dhambi ya asili, hivyo basi ubatizo ni njia mojawapo ya kusafisha dhambi ya asili.

Vile vile Bwana wetu Yesu Kristo alikufa msalabani kwaajili ya dhambi zetu. Tumekombolewa..

******** ******

Maandiko yanasema anaetenda dhambi hatauona ufalme wa Mbingu.. Tuzitii na kuzifuata amri za Mungu.

Hivyo basi ukifikiria kwa haraka waweza sema nao watauona ufalme wa mbingu endapo tu hawatatenda dhambi. "Atendaye dhambi si mwana wa Mungu".


Lakini bado unajiuliza " Hawa watu si wana dhambi ya asili"
Waliyozaliwa nayo na wanahitaji kubatizwa.
Je, watauona Ufalme wa mbingu pasipo kuondolewa dhambi ya asili kupitia ubatizo?

Na kama Yesu Kristo alikufa msalabani kwaajili ya dhambi zetu, Tukakombolewa!
Kama wokovu huu ulihusisha dhambi ya asili basi nao pasipo kutenda dhambi watauona Ufalme wa Mbingu.

Mambo ya Imani ni magumu, kila unachofikiri kuhusu uwepo wa Mungu na mambo yote yamuhusuyo hupati jibu.

Basi naweza sema hakuna ajuae kiama chetu sote ila Mwenyezi Mungu pekee.
Umefikiri vema mkuu, jipe muda uchambue imani nyingine kimya kimya kwa manufaa yako tu
 
29417662_931497287029415_5681226956390006784_n.jpg
 
Back
Top Bottom