Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jumamosi ilionekana kama Man City tayari imeshabeba ubingwa huo baada ya kuongoza 2-0 hadi kipindi cha kwanza dhidi ya mahasimu wao hao, lakini kipindi cha pili, Paul Pogba na wenzake walicharuka na kufunga mara tatu kutibua sherehe iliyokuwa ifanyikE huko Etihad baada ya mechi hiyo
 
Man City bado inaoongoza kwa tofauti ya pointi 13 na mechi zimebaki sita, lakini kwa matokeo hayo, inapaswa kuwa makini kwelikweli kwani ikiteleza inaweza kufanya mchakato wa ubingwa kuchukua wiki nyingi zaidi. Kimsingi lini hasa Man City itabeba ubingwa huo wa Ligi Kuu England msimu huu?
 
Ikiifunga Tottenham Aprili 14

Baada ya mechi yake ya leo Jumanne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool wakati itakapojaribu kupindua matokeo ya kipigo cha mabao 3-0, Manchester City itarudi kwenye Ligi Kuu England Jumamosi ijayo kucheza na Tottenham Hotspur.
 
Man City ina mechi ngumu sana wikiendi ijayo, itakwenda nyumbani kwa Tottenham na ikifungwa kisha Man United ikashinda mbele ya West Brom, basi itafanya pengo la pointi kupungua na kuwa 10, huku mechi zijiwa zimebaki tano, sawa na pointi 15. Man United ina rekodi kuwahi kupangua pengo kubwa la pointi kama hilo katika msimu wa 1995-96 ilipoachwa pointi 12 na Newcastle United kisha ikabeba ubingwa.
 
Man City bingwa Aprili 22

Kama Tottenham itaichapa Man City kisha Man United itaichapa West Brom, mambo yataingia kwenye wikiendi inayofuatia, Aprili 18 kuona matokeo yatakavyokuwa. Siku hiyo, Man United itacheza na Bournemouth. Man United kama itakubali kupoteza mechi hiyo au kutoa sare tu na Man City ikaibuka na ushindi dhidi ya Swansea City, Aprili 22 basi hapo itakuwa imetangaza ubingwa kwa sababu itakuwa imerudisha pengo la pointi 13 au 12 huku mechi zikiwa zimebaki nne, sawa na pointi 12. Man City ina mtaji mkubwa sana wa mabao hilo ndilo litakaloifanya kutangaza ubingwa. Lakini, itakuwa vizuri zaidi kama Man United itachapwa na Bournemouth kisha Man City ikashinda kwa Swansea.
 
Ubingwa Aprili 29

Vita hiyo ya mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England itafikia huko Aprili kama Man United itashinda mechi zake mbili itakayocheza hapo kati dhidi ya West Brom na Bournemouth, kisha Man City ikafungwa na Tottenham na kupoteza au kutoa sare pia kwa Swansea City. Kama hilo litatokea kama kutakuwa na matokeo hayo, hivyo Man City itawabidi kusubiri hadi Aprili 29, siku hiyo Man United itakuwa na mechi ngumu dhidi ya Arsenal Old Trafford, wakati Man City itacheza na West Ham United ugenini.
 
Hapo Man City itatangaza ubingwa kama itaichapa West Ham na Man United ikachapwa au kutoa sare tu na Arsenal kwani hapo kutakuwa na mechi tatu za kuchezwa na pengo la pointi litakuwa pointi 10 au tisa, ambazo zitatosha kuipa Man City ubingwa kwa kuzingatia mabao yake mengi. Suala la Man City kubeba ubingwa mapema litagemea zaidi na matokeo ya wikiendi ijayo, kama itafungwa, basi itaibidi kusubiri kwa wiki mbili zaidi.
 
ULITOKEA mtikisiko hasa Uwanja wa Anfield, nyumbani kwa Liverpool katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) dhidi ya Manchester City, na majogoo waliwararua Man City mabao 3-0.

Man City wanaosubiri ushindi mmoja kutangazwa mabingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) walipoteana kabisa na baada ya hapo wakaja kuzabwa na Manchester United waliowacheleweshea sherehe za ubingwa.
 
Sioni uwanja wowote wa London kuja kuwa na hali ile ya hewa na homa kubwa kama Anfield. Si uwanja mpya wa Tottenham unaojengwa wala ule wa Chelsea utakapokarabatiwa na kupanuliwa. Anfield palikuwa pa aina yake.
 
Spurs wakikamilisha mambo yao wataanza kutoa tiketi za msimu kuanzia msimu ujao, na inavyoelekea kutakuwa na utalii zaidi hapo pamoja na shughuli za wakubwa za kishirika, lakini wale watazamaji wa kawaida wadogo wanaweza wakashindwa kuhudhuria mechi mara kwa mara, kwa sababu ya bei.
 
Kumbe hata pamoja na kwamba watakuwa na uwanja wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 62,000, na kuwa na jukwaa moja kubwa zaidi Ulaya kote kwa kuchukua watu 17,500 upande wa kusini, haitarajiwi kabisa kwamba hali ya hewa inaweza kuja kuwa kama Anfield ambako kunajaa sana na washabiki wakiwa na shauku ya aina yake, achilia mbali fujo zao.
 
Mashabiki wa klabu za London wameanza kulalamikia kuongezwa kwa bei ya tiketi; tuliona jinsi wale wa Arsenal licha ya kununua tiketi wakisusa kuingia Emirates kutokana na mwenendo mbaya wa timu nab ado klabu zinaongeza bei kwa kati ya asilimia 25 na 50 huku uchumi ukiyumba.
 
Back
Top Bottom