Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

852737443_162287.jpg
 
Niliwahi kusoma mahala zamani kuhusu hili suala. Halina misingi katika sayansi ya ubongo bali wamekazia sana Eureka moment - ile moment ambapo jiniazi anajiwa na utatuzi wa tatizo lililomsumbua kwa muda mrefu kwa ghafla! Archimedes - yule mwanasayansi wa kale wa Athens - alipata suluhisho la jinsi ya kupima ujazo wa irregular shapes (taji la mfalme aliyekuwa amedhulumiwa dhahabu na sonara mkorofi) akiwa anaoga kwenye swimming pools za umma mjini Athens. Kwa furaha aliyokuwa nayo alivuvumka kutoka majini na kuanza kukimbia barabarani uchi huku akipiga makelele Eureka! Eureka! Eureka! (Nimegundua! Nimegundua! Nimegundua!). Watu wa Athens walipomuona walifikiri kuwa ameehuka. Na huu ndiyo ukawa mwanzo wa imani kuwa hawa majiniazi wengi huwa wana kaukichaa vichwani mwao.

Wanasayansi wengi mashuhuri pia waliendeleza kuipalilia imani hiyo angalau kimwoneko wa nje. Albert Einstein akiwa amebanwa na minadharia yake ile migumu migumu alikuwa hawezi kulala wala kula na hata kuoga. Kuna kipindi aliumwa kidogo afe kwa sababu tu mahesabu yalikuwa yamegoma kuendana na nadharia yake mojawapo. Minywele ile nyang'anyang'a mpaka watu wakaanza kusema pengine kawehuka.

Nikolas Tesla alijifungia hotelini New York na alikuwa hataki kuonana na watu hovyo hovyo mpaka akafariki peke yake. Isack Newton alikuwa na tabia za ajabu ajabu na alikuwa anapenda sana bifu na wanasayansi wenzake. Yaani ukimkosoa kidogo tu basi unalo. Marie Curie alikuwa kama roboti mpaka anakataa chakula kisa tu anakesha kwenye majaribio yake ya nguvu za mnunurisho mpaka anakufa alikuwa amekondeana kutokana na madhara ya radiation pamoja na pumu na wengine walidai kuwa alikuwa ameehuka...

Majiniazi wengi wana nguvu ya ajabu na inapowajia basi huwafanya wafokasi kwenye jambo linalowasumbua kwa nguvu zote haijalishi kama ni kuacha kula, kuoga, kulala na vitu vingine vya kawaida. Inakuwa kama vile wanaona maono ndiyo maana wengine wamekwenda mbali zaidi na kudai kuwa pengine huwa wanafunuliwa maono hayo na miungu (aliens). Wapo wengi wanaoamini kuwa Isaak Newton, John Maxwell, Albert Einstein na mwanahisabati mmoja wa India (nimemsahau jina) hawakuwa binadamu wa kawaida kulingana na upana, upya na umuhimu wa kazi zao katika ulimwengu wa kisayansi.

Samahani kwa kuandika gazeti mkuu...[emoji124]‍♂️[emoji124]‍♂️[emoji124]‍♂️
Nimelipenda gazeti ni miezi mingi haujafafanua kitu murua kama hiki keep it shimba upo vizuri
 
Ahahaha, hamna haja ya samahan hapo brotherhood, nikupe tu hongera maana wewe mwandishi mzuri sana na asanteh kwa ufafanuzi yakinifu......
 
Back
Top Bottom