Naamini kwa mashabiki wetu na sisi wenyewe, tutafikia mafanikio fulani,” alisema Hazard.
“Bado tupo kwenye Kombe la FA na tunahitaji kuleta taji Stamford Bridge mwishoni mwa msimu. Unapokuwa Chelsea itahitaji ucheze Ligi ya Mabingwa Ulaya kila mwaka, lakini mwaka jana hakutucheza na tulishinda ubingwa wa ligi, hivyo wakati mwingine kitu kibaya kinaleta kitu kizuri. Hata hivyo, hatujakata tamaa tunacheza kwa ajili ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kuna mechi sita zimebaki kwenye ligi na tutajaribu kufanya kila tunaloweza hadi kufika mwisho wa msimu.”