Pia, alifafanua kuwa kumbi hizo kwa sasa zina wanawake ambao wanafanya biashara ya ukahaba, jambo ambalo linachafua taswira ya Zanzibar.
Kufuatia uwapo wa hali hiyo, Mahmoud ameamua kuzifungia kumbi mbili za starehe za Ngalawa na Bwawani kwa kile alichokiita kukiuka makubaliano.
Mkuu huyo wa mkoa aliwataka wazazi na walezi kufuatilia kwa kina maendeleo ya watoto wao shuleni, kwa kuwa bila ya ushirikiano baina yao na walimu hakutakuwa na maendeleo.
Aliendelea kufafanua kuwa katika matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne kwa mwaka jana, kuna shule mbili ambazo zimeshika mkia ambayo ni aibu.