Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi hao wamesema kurudi katika nyumba zao ni lazima kwani hawana sehemu nyingine za kwenda.
"Tulikuwa tunasikilizia jana na leo, lakini dalili inaonyesha hakuna mvua kubwa itakayoleta mafuriko na leo tunatoa maji ndani turudi," amesema Asha Haule mkazi wa Kiwalani.
Amesema enea lao halipo bondeni wala mazingira hatarishi bali ubovu wa miundombinu katika eneo hilo umesababisha maji kujaa kila sehemu.
Mkazi mwingine mtaa wa Kizinga, Lucas Zacharia amesema kwa sasa hali inaridhisha huku akijipa imani kuwa mvua haitonyesha yenye madhara tena kama ilivyokuwa mwanzo.
. The Right to Democracy. We all have the right to take part in the government of our country. Every grown-up should be allowed to choose their own leaders.
Tangu juzi tunalala nje, baridi kali, tukisubiri mvua ikate ili turudi nyumbani, kwa hiyo leo tunatoa maji kama unavyoona vyumba vyote vimejaa, ila hadi jioni tunamaliza," amesema.
Katika hatua nyingine wakazi hao wameiomba Serikali kurekebisha miundombinu ikiwemo kuzibua mifereji ya kupitisha maji, ili kuepuka hasara zitokanazo na mvua kila mwaka.
Social Security. We all have the right to affordable housing, medicine, education, and childcare, enough money to live on and medical help if we are ill or old.
Wakati Jiji la Dar es Salaam likikabiliwa na mafuriko ya mara kwa mara kutokana na mvua, waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema wameanza mapitio ya mpango mkuu wa jiji hilo.
Waziri Lukuvi alisema hayo jana alipozungumza na Mwananchi alipotakiwa kufafanua kauli ya mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka aliyesema ili kuliepusha jiji hilo na mafuriko inapaswa kurejea master plan (mpango mkuu) ya mwaka 1979.
Profesa Tibaijuka aliyewahi kuwa waziri wa wizara hiyo, alisema Jiji la Dar es Salaam linajengwa kisiasa jambo ambalo haliwezi kuwasaidia wakazi wa maeneo yanayoathiriwa na mafuriko badala yake ifuatwe sheria licha ya kuwa itakuwa ngumu.
Alisema ili kwenda mbele ni lazima kurejea master plan ya 1979 ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere.
Nilipokuwa ardhi (wizarani) nilijitahidi kuokoa Bonde la Msimbazi kwa mujibu wa master plan ya 1979. Call it the Nyerere master plan (uite mpango mkuu wa Nyerere). Sikufanikiwa. There was no political will for it (hapakuwa na utashi wa kisiasa). Bonde likaendelea kujengwa. Kwa hiyo maji hayana njia za kufika baharini,” alisema Profesa Tibaijuka.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.