Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Watu wakumbuke hata kipindi cha Makamba (Yusuf) alipokuwa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam yalitokea na wakaokoa watu kwa kutumia helikopta katika eneo hilo, lakini walirudi tena hivyo suala la kumbembelezana lingeachwa katika kipindi hiki,” alisema.
 
Ufafanuzi wa Waziri Lukuvi

Waziri Lukuvi alipotafutwa na Mwananchi kuzungumzia ushauri wa Profesa Tibaijuka alisema Serikali imeanza mapitio ya master plan mpya ya Jiji la Dar es Salaam.

“Tayari tumeshapiga picha ya angani inayoonyesha jiji zima la Dar es Salaam na hii ni hatua ya mwanzo kabisa tuliyoifanya mwaka jana inayotusaidia kuandaa master plan ya Dar es Salaam,” alisema Lukuvi
 
Ufafanuzi wa Waziri Lukuvi

Waziri Lukuvi alipotafutwa na Mwananchi kuzungumzia ushauri wa Profesa Tibaijuka alisema Serikali imeanza mapitio ya master plan mpya ya Jiji la Dar es Salaam.

“Tayari tumeshapiga picha ya angani inayoonyesha jiji zima la Dar es Salaam na hii ni hatua ya mwanzo kabisa tuliyoifanya mwaka jana inayotusaidia kuandaa master plan ya Dar es Salaam,” alisema Lukuvi
 
Lukuvi ambaye pia ni mbunge wa Ismani (CCM) alisema, “Picha hiyo inatusaidia katika kuandaa master plan hiyo. Master plan ya miundombinu nayo inaendelea, picha hii ya anga tuliipiga mwaka jana na tumeisambaza ili mipango midogomidogo inayotekelezwa izingatie mipango miji.”

Alisema picha hiyo inasaidia kujua yote yanayotokea akisisitiza baada ya maandalizi ya master plan kukamilika wataipeleka kwa wadau ili watoe maoni.
 
Akichangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya ofisi ya Makamu wa Rais bungeni jana, mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Dk Immaculate Sware alizungumzia mafuriko jijini Dar es Salaam akitaka ofisi hiyo iangalie njia ya kumaliza tatizo hilo ili kuepuka maafa makubwa.

Dk Sware alisema kauli za kisiasa si wakati wake sasa, badala yake wakutanishwe wataalamu ili kutoa pendekezo la kumaliza tatizo hilo na kuwanusuru wananchi.
 
Mkazi wa Upanga jijini Dar es Salaam, Hashim Ismail akizungumza na mwandishi wetu alisema kwa mara kadhaa wamekuwa wakiiandikia barua Manispaa ya Kinondoni ili kupunguza mikoko eneo la Daraja la Selander lakini hilo halitekelezwi, hivyo kuwa chanzo cha maji kutopita kwa urahisi kwenda baharini.

Mwenendo wa mvua

Baada ya siku tatu za mvua mfululizo zilizosababisha balaa, jana hali ilianza kurejea kawaida maji yakipungua na barabara kupitika bila matatizo jijini Dar es Salaam.
 
Hata hivyo, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitoa taarifa ikisema mvua kubwa inayozidi milimita 50 itaendelea kunyesha katika maeneo ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara na visiwa vya Unguja na Pemba.

“Wakazi wa maeneo yaliyotajwa wanashauriwa kuendelea kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa na tahadhari zinazotolewa,” ilieleza taarifa hiyo

Kamanda wa polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alisema jana idadi ya watu waliokufa kutokana na mvua imefikia 14.
 
Alisema kutoka na mvua inayoendelea kunyesha na hasa Kisarawe mkoani Pwani imesababisha miundombinu yakiwamo madaraja yaliyopo mto Msimbazi kukatika.

Akizungumza na gazeti hili, meneja uhusiano wa Mamlaya ya Hifadhi za Taifa (Tanapa), Pascal Shelutete alisema mvua kubwa iliyonyesha ilisababisha baadhi ya wanyama katika Hifadhi ya Ziwa Manyara kushindwa kuhimili na kutoka nje ya hifadhi. Jana simba alionekana maeneo ya Makuyuni.
 
Eneo hilo ambalo ni sehemu ya ikolojia ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara na Hifadhi ya Taifa ya Tarangire kwa sasa limekuwa na ongezeko la maji kutokana na mvua.

Wahifadhi jana mchana walionekana wakifanya jitihada za kumuondoa simba huyo pembezoni mwa barabara.
 
Back
Top Bottom