Watu wengi pamoja na mimi , tunapotaka kula tunakuwa na nia nzuri ya kula kiasi, lakini tukianza kula tunasahau na kula zaidi kwa sababu ya njaa tuliokuwa nayo.
Kitu cha kufanya , pakua chakula ambacho unaona kuwa kitakutosha kutokana na nia yako, halafu ondoka sehemu ya chakula. Halafu usijipime kila siku , kama mimi nilivyokuwa nafanya kila siku asubuhi nilikuwa napanda juu ya mzani , lakini ilikuwa inanikatisha tamaa, maana uzito niliona kama unaongezeka. Nikaacha. Kwa hio jipime kila baada ya mwezi .

Nakumbuka tulifundishwa na wazazi wetu kuwa sio vizuri kuacha chakula kwenye sahani, kwa hio ilibidi kumaliza chote . Lakini nakuambia kwamba sio lazima kumaliza chakula chote kama utakuwa unajisikia kutosheka acha. Na kwa nini upakue chakula kingi ? kwa sababu hata mbwa huwa wana bajeti zao na chakula chao huwa kinatengwa.