Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG-20180425-WA0030.jpg
 
YAANI kabla ya swala la Magharibi haijaswaliwa ama wale mashabiki wa kulialia wa Manchester United na Arsenal kupigana makonde wakati wakishangilia timu zao, hapa nchini kila mtu atakuwa na matokeo ya pambano la watani, Simba na Yanga.
 
Ndio, vigogo hao watalianzisha mapema jioni ya saa 10:00 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika kipute cha kukata na shoka, ambapo kila upande unaamini utaibuka na ushindi. Uhakika huo unatokana na hasa kwa kuangalia ubora wa vikosi vyao na maandalizi waliyofanya mjini Morogoro kabla ya juzi na jana kumalizia hapa jijini.
 
Huko mitaani wiki nzima kumekuwa na amshaamsha za aina yake, vijiwe vya kahawa na vile vya daladala vikichangamshwa na maneno ya kejeli, tambo na mikwara ya kufa mtu, Simba ikitamba kuwa Jangwani hawachomoki, huku Yanga ikitamba kuua Mnyama
 
Simba iliyomalizia tizi lao Uwanja wa Boko Veterani, inaongoza msimamo ikiwa na alama 59 na kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuta ukame wa mataji Msimbazi, baada ya misimu mitano mitupu, huku wapinzani wao ambao ni watetezi wakiwa nyuma yao.
 
Licha ya kwamba mchezo huu unaweza kuamuliwa kimbinu zaidi kwa kutegemea makocha Mwinyi Zahera na wasaidizi wake wa Yanga na Pierre Lechantre na Masudi Djuma wa Simba walivyowaandaa vijana wao, lakini mechi hii ni ngumu kutabirika kwa aina ya vikosi vitakavyotumika kwenye mchezo huo na yeyote akizubaa ataumia.
 
YANGA YAMALIZA KAZI

Katika kuelekea mchezo huo, Yanga jana asubuhi ilifanya mazoezi yao ndani ya kambi ya kijeshi kwa kujichimbia Chuo cha Polisi, Kurasini huku vijana wake wakionekana kuwa na mzuka zaidi na hasa kwa mavitu waliokuwa wakipewa na Mkongomani huyo.
 
Morali ya Yanga iko juu kwa kila mchezaji kujituma katika kila aina ya zoezi walilokuwa wakipewa na imeonyesha uchangamfu mkubwa kana kwamba, mechi hiyo ni ya kawaida kwao.
 
Zahera kila baada ya zoezi moja alionekana kuwaita wasaidizi wake na kubadilishana nao mawazo kisha kuingia katika zoezi lingine huku wachezaji nao wakionekana kushika kwa haraka maelekezo waliyokuwa wakipewa.
 
Utamu wa Zahera ni kwamba amekuwa akipambana kutumia lugha ya kiswahili kidogo kilicho na lafudhi ya kilingala ujanja ambao, uliwateka kirahisi wachezaji wake na kuelewa kile anachotaka huku pia Nsajigwa akisaidia zaidi kwa kufafanua kwa kiswahili fasaha wakati Mwandila akiwasaidia wengine wasiojua Kiswahili na kilingala
 
MABADILIKO KIDOGO

Katika sura ya kikosi cha kwanza Zahera na wasaidizi wake, wamefanya mabadiliko kidogo kwenye kikosi kilichocheza mechi ya mwisho akili inayoweza kuwa ni janja flani ya kuzuga Lechantre wa Simba.
 
Mara ya mwisho Lechantre kuisoma Yanga ni wakati ikitoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Singida United, Uwanja wa Taifa na kikosi hicho kimebadilishwa kidogo na kile cha leo.
 
Zahera huenda akawapanga ukuta utakuwa na Youthe Rostand akisaidiwa na mabeki Hassan Kessy, Haji Mwinyi, Kelvin Yondani na Andrew Vincent huku katika kiungo wanaoweza kupewa nafasi ni Said Juma Makapu, Papy Kabamba Tshishimbi, Yusuf Mhilu, Raphael Daud na washambuliaji ni Ibrahim Ajib na Obrey Chirwa.
 
Katika kikosi hicho huenda watu wawili wanaokosa ni Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Pius Buswita wanaweza kuingia katika mabadiliko ya pili wakiwa ndiyo wachezaji waliocheza mchezo wa mwisho.
 
Chenga nyingine aliotimua Zahera kuwahadaa Simba ni staili yao tofauti kidogo ya kutengeneza mashambulizi na pasi za haraka zinapigwa kisha ukifika mbele watu wa mbio wawili wanatakiwa kutengeneza mashambulizi ya haraka kwa Chirwa na akikukosa basi Ajib na Raphael wako tayari kumaliza mchezo.
 
Chenga nyingine aliotimua Zahera kuwahadaa Simba ni staili yao tofauti kidogo ya kutengeneza mashambulizi na pasi za haraka zinapigwa kisha ukifika mbele watu wa mbio wawili wanatakiwa kutengeneza mashambulizi ya haraka kwa Chirwa na akikukosa basi Ajib na Raphael wako tayari kumaliza mchezo.
 
Staili hiyo ikamuibua Dante akisema ni kama kazi ya maandalizi ya mchezo huo imeisha na kitu muhimu kwao ni kuja kwa Zahera, ambaye ndani ya siku chache wamemkubali na wanataka kuifanya kazi yake kuanza vizuri.
 
Simba siku zote tunaiheshimu, ujio wa kocha mpya kikosini kila mtu amekubali ni kocha anayejua kutengeneza wachezaji kisaikolojia ni kama Lwandamina (George) aliyeondoka tofauti yao ni mifumo tu. Kuna vitu ametupa kama tutatulia vyema wakitoka salama basi ni sare tu,” alisema Dante.
 
Back
Top Bottom