Hata hivyo Atletico haikuweza kuwa tishio sana kwa Barcelona. Kuna wakati Atletico ilikuwa nyuma kwa pointi tano tu kutoka kwa Barcelona, lakini ikajikuta ikianza kuangusha pointi kwa timu dhaifu kama Espanyol, Getafe na Las Palmas.
Baada ya Barcelona kuichapa Atletico katika uwanja wake wa nyumbani pengo baina ya timu hizo liliongezeka huku Atletico ikiendelea kuishiwa makali na mwisho Barcelona imeishia kuchukua ubingwa kiulaini.
Kocha Valverde aliendeleza vema sera yake ya kubadili wachezaji mara kwa mara na hata baada ya kumpoteza Neymar aliyehamia PSG katika dirisha kubwa lililopita, lakini bado walionekana kuwa timu imara ndani ya La Liga kuliko wengineo na mpaka sasa hawajapoteza hata mechi moja.
Kama ilivyo kawaida, staa wa Barcelona, Lionel Messi, ameendelea kuwa nyota zaidi wa timu hiyo msimu huu kwa mabao yake na pasi zake zilizozalisha mabao ya kutosha huku rafiki yake, Luis Suarez akiwa msaidizi wake wa karibu katika ufungaji.
Mastaa wengine kikosini kama Andres Iniesta, Ivan Rakitic, Jordi Alba, Gerard Pique, Sergio Busquets na Samuel Umtiti, na kikosi kizima wote wamekuwa katika ubora wao msimu huu, ingawa shukrani nyingine za kipekee ziende kwa kipa wao wa kimataifa wa Ujerumani, Marc-Andre Ter Stegen.
Kipa huyo anatazamiwa kupambana na kipa namba moja wa Atletico Madrid, Jan Oblak katika tuzo ya Kipa Bora wa msimu iitwayo Zamora baada ya kuruhusu mabao machache msimu huu.
Barcelona pia ilionyesha ukomavu mkubwa kwa kushinda mechi ngumu dhidi ya wapinzani wake.
Ilishinda Santiago Bernabeu dhidi ya Real Madrid na pia ushindi dhidi ya Valencia na Atletico pale kwao Nou Camp huku ikitoka nao sare ugenini licha ya wapinzani kuongoza mechi kwa muda mrefu.
Barcelona imeonekana kurudi katika fomu yake katika miaka ya karibuni. Ilitwaa mataji mawili mara tatu katika miaka ya 1950 lakini walilazimika kusubiri mpaka mwaka 1998 walipotwaa tena na kocha wa Kidachi, Louis van Gaal.
Na sasa Valverde amejiunga katika orodha ya makocha ambao wamewahi kuipa Barcelona mataji mawili na hivyo kuingiza jina lake katika historia nzuri ya klabu hiyo.
Andy Carroll ametimuliwa katika kikosi hicho, baada ya kuzozana na kocha wake David Moyes.
Mshambuliaji huyo wa West Ham United aliondolewa katika mazoezi na kutakuwa kurejea nyumbani kutokana na mzozo huo ambao Moyes amedai ni utovu wa nidhamu.
Mchezaji huyo aliwahi kutupiwa ndoano na kocha wa Chelsea Antonio Conte, aliyetaka kumsajili katika dirisha dogo Januari, mwaka huu kabla ya mpango huo kugonga mwamba.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.