Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

21A362AD-060D-433A-A4C1-F0E249768E12.jpeg
 
HUKO nje ni Real Madrid na wengineo, lakini ndani ya Hispania Barcelona ni mfalme wa zama hizi. Juzi Jumapili usiku ilitwaa taji la La Liga katika dimba la Estadio Riazor nyumbani kwa Deportivo la Coruna huku ikiwa imebakiza mechi nne.
 
Barcelona ilishinda mabao 4-2 ugenini kwa Deportivo ambayo ilishuka daraja baada ya matokeo hayo na mitaa ya Catalunya ililipuka kwa furaha kubwa baada ya tukio hilo.

Baada ya kutwaa Kombe la Mfalme wiki iliyopita, Barcelona sasa inakuwa imetwaa mataji mawili msimu huu na hii inakuwa mara ya nane kwa timu hiyo kutwaa mataji mawili kwa mpigo huku kocha, Ernesto Valverde na wachezaji wake wakiingia katika historia ya klabu hiyo.
 
Kwa msimu mzima Barcelona ilikuwa ikicheza katika sayari ya peke yake huku wapinzani wao wa karibu Real Madrid wakijutia kwa mwanzo mbovu wa msimu ingawa wanatamba katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambako wanatazamia kutinga fainali.
 
Back
Top Bottom