Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jumatano saa 4:00 asubuhi, tunakaribishwa ndani kwa sauti za vilio na nyuso za majonzi zikiwa zimetawala. Ni katika familia ya Magreth Ruben na mumewe Michael Nzilalila iliyopo mtaa wa Muungano, Kata Tungi wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Magreth amekumbatia picha kubwa ya mtoto aitwaye Joshua Michael (2), akiwa katika sura ya tabasamu huku akitiririka machozi na sauti yake inatoka kwa huzuni sana tangu alipopokea taarifa za kuuawa kwa mwanaye kwa kuchomwa na kisu tumboni na kisha kufichwa kwenye uvungu wa kitanda chake.
 
Uhai wa Joshua aliyezikwa katika kijiji cha Nyabila, wilayani Sengerema siku ya Ijumaa wiki iliyopita, umekatizwa na mtoto wa dada yake Magreth aitwaye Deta Kalambo (19), aliyekuwa akiishi naye hapo nyumbani kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.

“Niliishi naye kwa upendo, sikuwahi kumfanyia kitu kibaya, nilimnunulia nguo nzuri kama mtoto wangu. Nilimjali, nikamsomesha ufundi chereheni, aliingiza mpenzi wake ndani ya nyumba yangu nikamsamehe, sikumuadhibu, leo anamuua mwanangu, ehhee,” anapumua kwa uchungu huku machozi yakimtoka.
 
huzuni kubwa....
 
Mama Joshua ni muuguzi katika Hospitali ya Vikindu, iliyopo Mkuranga, Pwani na mumewe ni mfanyakazi katika kampuni ya ununuzi wa mazao ya biashara Agri Venture kwa hiyo Deta alishinda muda wote na mtoto Joshua nyumbani kwa ajili ya uangalizi.
 
Nzalalila aliporejea Jumatatu akitokea Tanga kikazi anakutana na msiba wa mwanaye. Mama anaondoka asubuhi nyumbani salama lakini jioni anakutana na barua ya Deta yenye kurasa mbili za utata wa kupotea kwa mtoto wake, kumbe tayari ameshamuua.
 
Sura tatu za Deta

Deta binti mwembamba, mrefu wa kabila la wasonjo wa Arusha, alimaliza darasa la saba mwaka 2015 kabla ya Mama Joshua kumchukua na kuishi naye kama mtoto wa familia hadi alipojifungua mtoto wake wa pekee, Joshua.

Mama Joshua anasema hakuwahi kuona dalili za ukatili wowote kwa Deta dhidi ya Joshua na walikuwa wakifurahi hadi siku ya mwisho kuachana naye.
 
Mama Joshua na Deta aliyekuwa mwanafunzi wa kozi ya ufundi chereheni chini ya Fundi Alex, eneo la Tungi Magengeni, Kigamboni, walikuwa waumini Kanisa la Jesus Christ Miracle Center, lililopo Tungi chini ya Mchungaji Somwe Patauli.

Mchungaji Patauli anasema Deta alikuwa muumini wa kanisa lake na alikuwa akisumbuliwa na mapepo ya ukoo, huku Baba Joshua akithibitisha tatizo hilo la mapepo na aliwahi kushuhudia akidondoka kanisani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…