Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2018-04-21-19-15-36.jpg
 
........Kabla ya Vita Kuu ya Kwanza duniani, Edward Spiro (mwenye asili ya Kiyahudi, aliye na uraia wa Austria), alikuwa mmoja wa mawaka wakubwa wa Shirika la Ujasusi la SIS (British Secret Intelligence Service-M16). Wakati huo akiishi kwa kufanya kazi ya Uandishi wa Habari wa Kujitegemea, akiandikia magazeti mbalimbali ya nchi hiyo. Mahusiano ya Spiro na SIS yalianza nchini Austria baada ya kuhitimu katika Chuo kikuu cha Vienna, wakati huo akiwa mhariri wa masuala ya siasa wa gazeti moja la jioni la nchi hiyo. Mnamo mwaka 1936, Spiro alifanywa kuwa Chanzo cha Taarifu wa SIS na aliyekuwa mkuu wa kitengo cha shirika hilo nchini Austria, Kepteni Thomas Kendrick. Ilikuwa ni fursa ya ushushu iliyomuwezesha kuikimbia nchi hiyo na kuwa mkimbizi nchini Uingereza.

Kama Wayahudi wengine waliokimbilia nchini humo, Spiro hakuwa na japo senti moja katika mfuko wake. Kwa hiyo alihitajika kufanya kazi ya ziada katika awamu hii ya maisha ya ukimbizini. Kabla ya kujificha katika mwavuli wa uripoti wa gazeti la Daily Telegraph katika bunge la nchi hiyo. Spiro alijipenyeza kwenye makundi ya Manazi (mafuasi na makada wa Chama cha Nazi kilichoasisiwa na Adolf Hitler), akwajibika vema katika shughuli yake ya siri ya uajenti wa SIS. Jukumu lake katika makundi hayo kama wakala, lilikuwa kupeleleza wanachama walio mstari wa mbele na majasusi waandamizi wa Kinazi waliomo kwenye makundi hayo. Akiwa mmoja wa wanachama kindakindaki walio mstari wa mbele, akifahamika kwa jina la E.H.Cookridge, Spiro aliajiriwa kwa kazi ya propaganda katika Wizara ya Ustawi wa Uchumi ambayo ilikuwa Idara ya serikali ya nchi hiyo iliyokuwa ikirusha propaganda dhidi ya Ujerumani.

Baada ya Vita Kuu ya Pili kumalizika mnamo mwaka 1945, katika kitabu chake kilichoitwa, "Ujasusi Pandikizi", Spiro aliandika kwa mapana sana, Taaluma ya Ujasusi akielezea maisha ya ushushushu ya Kim Philby na George Blake. Spiro alieleza katika kitabu hicho kuwa alimfahamu kwa mara ya kwanza Kim Philby mjini Vienna mwaka 1933, wakati huo wote wakiwa wafuasi wa harakati za chini chini zilizokuwa zikipinga udikteta.

Akiwa Chuo kikuu cha Vienna, Spiro anasema alikuwa akichukua masomo ya Sayansi ya Siasa, wakati huo huo, akiwa ripota/mwandishi katika gazeti moja, toleo la jioni kabla baadaye kuhamishiwa toleo la asubuhi. “Kitaaluma, magazeti ya asubuhi huhitaji umakini zaidi kwa sababu bongo za wasomaji huwa tulivu kulinganisha na magazeti ya mchana. Kwa hiyo, sisi waandishi wachanga tuliwekwa kwenye magazeti ya mchana, ”Spiro alieleza. “magazeti hayo hayakuwa yakimilikiwa na Chama cha Social Democratic lakini yalikuwa yakiziunga mkono sera za chama hicho kama magazeti ya Daily Herald na Daily Mirror yalivyokuwa yakikiunga mkono Chama cha Labour (…) Baadaye nikawa mwandishi wa masuala ya Bunge na baadaye tena nikiwa na umri wa miaka 25, nikawa mhariri wa masuala ya Siasa wa gazeti hilo.”

Akiwa mwanafunzi, Spiro alieleza kuwa alikuwa mwanachama wa Klabu ya Social Democrat iliyokuwa chuoni hapo kisha akawa mmoja wa viongozi wa Klabu hiyo iliyokuwa na mrengo wa mageuzi na baadaye tena akawa mwanachama wa kawaida. “Mnamo mwezi Februari, gazeti letu lilifungiwa na wahariri wote wakawekwa rumande. Mimi nilikuwa mmoja wa waliowekwa mahabusu, pamoja nasi walikuwemo baadhi ya wanasiasa,” Spiro alisema. “nikilinganisha na uzoefu wangu wa ufungwa katika magereza ya Dachau na Buchenwald miaka kadhaa iliyopita, mahabusu ya Wollersdorf, niliiona kama ni mahali pa mapumziko.” Spiro aliachiwa wiki chache baadaye baada ya kukosekana ushahidi wa katika kesi iliyokuwa ikimkabili, ya kutaka kufanya mapinduzi.

Hata hivyo, Spiro alijikuta hana kazi baada ya magazeti yote ya Wajamaa na Maliberali kufungiwa yakidaiwa kuandika uchochezi dhidi ya serikali. “Nilifanikiwa kupata ajira katika kampuni moja ndogo ya uchapishaji wa vitabu vya sanaa. Hapo nikiajiriwa kama mhariri wa vitabu na niliwekwa katika bodi ya uhariri, nikishauri na kupitia vitabu kabla havijachapishwa (…). Siku moja nikiwa ofisini kwangu, alikuja Pilby kunidokeza kuwa angeweza kupata nyumba isiyo na wasi wasi kabisa ambayo tungeitumia kufanya mazungumzo ya siri. Nyumba hiyo mmiliki wake alikuwa mama mmoja wa Kingereza aliyekuwa akiitwa Mary (Mary halikuwa jina halisi, jina lake lilikuwa Muriel Gardiner). Mary alikuwa mtalaka wa tajiri mmoja wa Kimarekani, na alikuja Vienna mwaka 1927 kama mwanafunzi wa udaktari (utabibu).

“Mama huyo alikuwa na kitita cha pesa, akimiliki msitu wa miti ya mbao na akiendesha mradi huo uliokuwa jirani na Chuo Kikuu cha Vienna. Kujitolea kwake katika harakati za Wasoshalisti kulimfanya asiweze kuishi maisha ya kifahari. Alikuwa mama jasiri na mkarimu na mara nyingi alikuwa akisisitiza kulipwa kwa wahudumu ambao Halmashauri Kuu ya Chama cha wasoshalisti hakikuwa kikiwajali. Pilby alijifanya ni yeye aliyemshawishi Muriel ajiunge na harakati zile lakini baadaye nilikuja kufahamu kuwa mama huyo aliingizwa katika chama hicho na Ilse Kulczar, mmoja wa viongozi wa ndani kabisa wa harakati hizo. Baadaye nilikuja kufahamu kuwa Pilby alikuwa mpelelezi pandikizi/pacha ambaye wakati akisaidia harakati za makundi ya Masoshalisti alikuwa pia akijihusisha na upande wa wapinzani, Makomunisti.”

Sasa tuachane na Spiro, tuje kwa jasusi pandikizi/pacha mwingine. Naye si mwingine bali ni Sidney Reilly. Sidney ni mtu aliyesababisha kutungiwa vitabu na filamu za James Bond. Huyu ni jasusi ambaye aliwahi kuishi kipindi fulani katika karne ya 20, akifanya kazi katika serikali nyingi. Alijulikana kama Ace of Spies. Alikuwa mtu hodari kwa uwongo, ulaghai, kujipaisha na kujipachika vyeo. Taarifu nyingi kumuhusu yeye hazieleweki sana lakini inajulikana kwamba, aliweza kuvuka mipaka ya nchi nyingi kutumia majina ya watu wengine na kufanikiwa kuiba siri nyingi za jeshi, majengo na ramani za ndege. Pia alikuwa mtongozaji mweledi maana aliweza kupata wake wengi wa maofisa wa jeshi, wanasiasa na wengine maarufu kulala nao kisha kuchukua siri alizokuwa anazitaka. Kazi yake kubwa aliifanya mwaka 1917, ambapo aliteuliwa na serikali ya Uingereza aende Urusi kuangusha serikali ya Bolshevik lakini ilishindikana. Kisha akafanya jaribio la kumuua Vladimir Lenin , lakini kundi lake lilijulikana, haraka kama kipanga, alifanikiwa kutorokea Finland baada ya kutumia jina la Mjerumani mmoja. Alihukumiwa kifo wakati akiwa mafichoni mwaka 1925, ambapo alidanganywa na dada mmoja kurudi tena Urusi ndipo alipokamatwa. Ingawa hakuwahi kukiri kuwa yeye ni jasusi lakini aliuawa kwa kupigwa risasi............

Kwa undani zaidi soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi. Kwa 80,000/= tu.

+255715865544, +255755865544

Na Yericko Nyerere
 
Back
Top Bottom