Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hata hivyo, biashara ya ubia imesababisha baadhi ya watu kugombana kiasi cha kusababisha wengine kulipiza visasi kwa kuuana, jambo ambalo kwa mila na desturi za Tanzania halikubaliki.

Suala la kuchagua rafiki wa kushirikiana katika biashara linatakiwa kufanywa kwa umakini mkubwa na uangalifu, ikibidi lihusishe watu wanaoheshimika katika jamii kwa ajili ya kutoa ushauri juu ya mshirika mwenza kama kweli anafaa au la.
 
Pia, ni vema mnapoamua kuanzisha biashara mkaingia makubaliano ya kisheria juu ya namna ya uendeshaji wa biashara yenu, mgawanyo wa mapato kulingana na mtaji mliowekeza, menejimenti yenu itakavyokuwa na kama mtaajiri watu wa kusaidia katika uendeshaji wa biashara.
 
Ili kuepuka athari zinazoweza kuharibu biashara na urafiki wa washirika katika biashara ni lazima kila mmoja akachukulia kazi yake kwa hisia kuwa bila rafiki yake asingepata hicho alichonacho sasa, hivyo aheshimu kila fedha inayopatikana igawanywe kwa usawa kulingana na mwongozo waliokubaliana.

Ni vizuri pia biashara ikarasimishwa ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza baadaye baina ya wahusika, lakini pia kila mmoja akumbuke kulipa kodi na tozo stahiki zilizopangwa kwa ajili ya kuboresha biashara yao.
 
852902332_28182.jpg
 
Back
Top Bottom