Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pia, wapo marafiki walioamua kuunganisha nguvu pamoja na kufanya biashara kwa mafanikio makubwa kiasi cha kuwa mfano wa kuigwa katika jamii wanazoishi, licha ya kukutana na changamoto za hapa na pale katika biashara, lakini bado waliweza kusimama imara na kushinda vikwazo.
 
Ni muhimu kuchukua muda wa kutosha kujiridhisha kama kweli rafiki huyo unayetaka kushirikiana naye katika kuanzisha biashara anaweza kuheshimu na kutekeleza majukumu mliyojipangia katika kuanzisha biashara ili hatimaye muweze kukuza mtaji.
 
Awe mwenye kuridhika na kile anachopata badala ya kuwa na tamaa ya kupata sehemu kubwa ya faida inayopatikana hasa kwa kutumia hila na udanganyifu kama vile kudai aliuza bidhaa kwa bei ya chini wakati kiuhalisia aliuza kwa bei kubwa na ya juu iliyozalisha faida ya kutosha.
 
Awe mwenye kuridhika na kile anachopata badala ya kuwa na tamaa ya kupata sehemu kubwa ya faida inayopatikana hasa kwa kutumia hila na udanganyifu kama vile kudai aliuza bidhaa kwa bei ya chini wakati kiuhalisia aliuza kwa bei kubwa na ya juu iliyozalisha faida ya kutosha.
 
Mnapoanzisha biashara ni lazima kujua aina ya bidhaa mnazotaka kushughulika nazo. Ni biashara ya kusafirisha bidhaa ndani na nje, kuuza bidhaa dukani, kufuata bidhaa na kuuza kwa jumla kwa watu wenye biashara za rejareja.
 
Ni vyema kutazama nani amewekeza mtaji mkubwa na mpanglie njia bora ya kugawana faida kwa kuwa mgawanyo wa faida umekuwa mojawapo wa changamoto kwa baadhi ya marafiki waliokubaliana kuanzisha biashara ya pamoja, hasa kama mtaji uliotumika mwanzo kuanzisha biashara haulingani. Wapo baadhi ya watu hukerwa kuona mwenzake mwenye mtaji mkubwa akichukua mgawo mkubwa unaotokana na faida iliyopatikana, matokeo yake huingiwa na wazo potofu juu ya kutaka kujiongezea kipato kwa njia isiyo sahihi.
 
Uadilifu humuongoza mtu yeyote kuheshimu kazi yake, ataiheshimu na kutamani kuona akipiga hatua chanya katika kujiletea maendeleo yeye na rafiki yake, uadilifu utamfanya asafiri kwa ajili ya kununua au kuuza bidhaa bila kujali mshirika mwenza anafanya shughuli nyingine binafsi inayomwingizia kipato nje ya biashara yao.

Ni uadilifu pekee utakaomuongoza mtu kuuza au kununua kwa usahihi bila kudanganya ili tu ajiongezee kipato cha ziada na kumuacha rafiki yake asijue kama anaibiwa taratibu. Matokeo yake mtaji unaweza kuporomoka na kupelekea biashara kufa.
 
Back
Top Bottom